Sema Naye: Label 5
Headlines News :

NEWS

Latest Post

Showing posts with label Label 5. Show all posts
Showing posts with label Label 5. Show all posts

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria yaendelea na kazi zake Ofisi Ndogo za Bunge Dar

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, October 10, 2013 | 9:41 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEglm3OTjDA8dJOvScAZOwfjlvxZ6l2Si2bgdKwcN6jsGG-D162iRTVCXjH4QmxoqleGDZL6fF6eDP7S1lnAQMgYmAkjCsmOkp8QQVJPv51g7YTsrI1jbvFDP9BZ8uuerMgygV_jrK0L5a_o/s1600/A.JPG
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Pindi Chana (Mb) akifanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati wakati wa kupitia muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Miscellaneous Amendment Act 2013) wakati wa vikao vya kamati vinavyoendelea Ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2X175r4Cljjb1nRbS6rzQ8GhFZoB6pFYZaYvBcvtpNVb784k5cMOMYK8fTZGn_thxSqBtqaA3wtsOjkXUgCO4yO0CTIUGT0t25MxGcc5VXCvUVf_VbNvC14onl6siZx_46Lr_5oR-28sD/s1600/B.JPG
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. William Ngereja (Mb) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Pindi Chana (Mb) wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Miscellaneous Amendment Act 2013) Ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam leo.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-HlkxJbpssVESprD08mxS9lVVHRfzBRyovn2wPREX1NZpv5OxlFF6cSwTgeXp7vr40QosdUmfTjALq1KSoNHvVAFo_ck9v-mf0E-QQQpecbHmgNp63BQkdl9ugTxajPuIia-Z0T40xH6U/s1600/E.JPG
Mhe. Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo akichangia jambo wakati wa kamati hiyo.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuATq4yYH2mo12-Zpv2KOqslJSipFd1MLRBHYMBDlhlzzpOqVLeBgnGFDjkgSzjZwDLwmThAA04Dz2Sk6B9fsdsJH-6nPzhYCgiDixm1wHxHvbV5OPKlsxD1Gn9d7T25iB3q_iHkYsPbE3/s1600/F.JPG
Mhe. Mustapha Akunay (Mb) nae akichangia.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmQxe0ow6p1hf8IfGSu8zX5Gw7olCLrby7rA7rmWIZdRpHIHqWYFjnS_-X7svdok8-QXDlJokl_a8EKPrv2tChbxJ_GFJBA1JQqd7pyWlgdxybbz5MtXuoyNBOk2M1DjQp5O6k_WPPYYMC/s1600/G.JPG
Mhe. Abbas Mtemvu.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MAGUFULI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxcptv3FsGgQzBaVclFTlATy60R4fUakrCb6oss6QfVjJQJy_MHmgYHUm4Oir5QO9flyVmkVLSj95lcmGAVISCvkR-CvAhCgpRO_daDpq8w2uC7ngkKohj-1Wb-33hIZC4g5SzTut_VFj1/s1600/Picha+1.jpg
 Magari yakirekebisha uzito wa  mizigo baada ya kupimwa katika Kituo cha Mizani cha Mikese Mkoani Morogoro
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDBcwn0sbY3HDGAFx0QxlB9RqSRRsJTToCQvfqxaJffC83rg6xbzuMXSGzD3ywdPRXwWQMU0_V-jFRmD5mmhtA3HJBIJ93uJsFb31nuhB5XXgjuapAJUcmWzxe6nXvtpwS1WoJeG5mM3VU/s1600/Picha+2.jpgMagari yakiendelea kupimwa katika Kituo cha Mizani cha Kibaha mkoani Pwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggFq-iNwwtIEX5hB04KtV-Wd_hqjsTH8HkIPq2d_3ftGaJ6LWC5JoDghl-dBnIAJw1hFAlxd7dbmrOj5YLIo8XzZZfV_ettqG9Evr9tEN_-ZjcTuYW6JtFA1cOoUWZwAh1ybXkYTu2Q30W/s1600/Picha+3.jpg Gari likiondoka baada ya kupimwa katika mzani wa barabarani likiwa limezingatia ya uzito uliowekwa kisheria.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikHDE3pwXu3OFZbN7HD7eliMdWC3sk2xWa6SPMkmQkNYCq36Zyyx2LZGIJa1ecIFnsL9veC08hsN2j5NRiVvcs0yfifOYEiHj5IplMpGJ5RqSpMTEFaVhnlDFkx5ftdPzO7t9aAYdV1DO0/s1600/Picha+4.jpg Upimaji ukiendelea Kibaha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjewOMgJJxo7pUKyad3RGdlRsomnpJQD-XCXJO4modgx5UzagepTnMKLNJy2fqUjj9VhtSpeL3F-aSFinxZdX8r5JC254-SP1IATsyjAD-F2M0cUPe6BtR0-RFR2ruHd308b8S_vm3S92-X/s1600/Picha+5.jpg Barabara ikiwa imebonyea kutokana na uharibifu unaotokana na magari yaliyozidisha uzito zaidi ya viwango vilivyowekwa kisheria..

Mkutano wa 34 wa SADC-PF kufanyika Tanzania

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, September 24, 2013 | 2:55 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4jCrkaWvkbP75Mr_H-SOuVPtUkI8B5YrcKhnIt4_o11IYteIpENvzp-QS5zZaGM5PZpTcN_dPoWYQXOYadb4-uY7AJ-VuG3gWX6NcoMPoWU7XVpCb716-bmFk6JlQVTDICH9R4ZKQWt60/s1600/1.+KB+MEU.NGRDT+JPG.JPG
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashillila akiongoza Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa 34 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachana wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) mara baada ya kuwasili jijini Arusha na kukutana na wafanyabiashara wanaomiliki Hoteli jijini humo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhshNUnQCqJU3ZMoEoDrhdxDWEg52CKZGEv_jKtaAGLl6Sb1zjB72zq7DLsfbXsyWVSSx5j09Yk64mCt02ivZrA4hmGncEnZEOJY0MqaJOSfQ_KMkVNEn0HL6oqXRNRaAoFMlvxp-fp-6r/s1600/9.+KB-Ngrdt.JPGDkt Kashillilah akitoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge kabla hajaondoka Arusha kurejea Dar es Salaam.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpWYDDt37y_n-UPemBK077BXe9bG09JceDWU34xDfSBRxH20hFDlmMLSQsT3QeNy1wDDLKkjB8JtijzK7PW3GXuvzvRaIhJpNbhW_RcVQtVcuCHJ2Njc_kC1t8tXu6Kzs4UoHVajR1VGKj/s1600/5.NGRDT+.JPG
Kamati ya Maandalizi pamoja na wamiliki wa Hoteli Jijini Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqixM6Gid_jrfRi6VsbaB95coVz5HctY6Py0nm22jfKhwlLKAj-2Xhahr3dkU-vGVNhuxicFRv1PeR9_fjTxiYAyX6RuymoVgoVSejTzEp2P_bK-jgnHN-VDBsyva6TiNdr_e5zMtbaFq-/s1600/3.+NGRDT+Cotages.JPGMoja ya majengo ya Hoteli za Arusha. Mikutano ya Kimataifa ni moja ya viashiria vya kutangaza Tanzania ulimwenguni.

WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVZz4p9t_GqnoQj22o-7gzUvV9f8CjdOn0u8MQ16vnO-HiUCWfiNTL-rrQqnkesGUp6WL3kmqYv9E4LX1TCHu7atna7sJWuKJWTf-TRvsHa37FefAgAFm7cZTHyA1XMqZHDx_aH-dUz1Xm/s1600/PICHA+1.jpg 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiTl4VZ4PQP58U6S7kDqc4Dm3sfNoWttzGbi4ugzxyf3Ju2kOusLxudL1hXp2ZKj5sNeE8-6KRPQeYvQImonkbeRLLho7kd5LyppqtfYCV-Nye3qdfs0OVCx1_BIjQ3_H70p5lhFV9uSbA/s1600/PICHA+No+2.jpg
Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine alioambatana nao.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,  leo ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya,  kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba 2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na Hospitali ya MP Shah.


Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

ZIARA YA DKT MWAKYEMBE NCHINI MAREKANI


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIOaVCIJ270BG2e_31eQu5nOYk-3Ak-G6BqyLxGDrNevp_5pYtjeAfNuvVfWThJFd1r3ufB7IwMRIqhCldlw135-svwuuiYluCD5C_iyKAIv1c23NOObrHbV_oixG_WZtarG0_l2lV-Mjh/s1600/MWAKYEMBE+1.jpgMhe. Harrison Mwakyembe alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House, Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo (wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia).

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLhsuVP5lGDiyJmmaO7iBPD-a_wRHm3QGPGw8hRoYiYmpOWLGgGGfcoS3WlBHGnaxU4jpRHA_7ZXcvkbbvLD97snJKcKDNxDzdraedy3ItcrxwHOEy37v1zHZzHaFuTYdt2GhaQWQdgb-z/s1600/mwakyembe+6.jpgMhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya kuwasili hotelini alikofikia.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixbqQAL8tFfUf7PR7HQgrk_RVY_NmTc1P-5WDXvYr8fM0YD6KazELfHO5YnJ310AgxKpsYvh3VIhlR32CL5kaORgjt58bWATLIO-jcnXmx00O3Cm3t7-K00JpxiHgsa-42f1Wbw2ZEfE6S/s1600/MWAKYEMBE+3.jpgMhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHMFzcoCBr7_2UmadAOqygtzXcwTJpeczU6SC15Ige1rgzjeBIXMioq_qXHGPdC8GbUNaqSlL702udLXItEXl73-4ibCKI42CjykqKiIhFXubQ9e2q_-s4tVlCt6wlZxyER9_OukxfcNRK/s1600/MWAKYEMBE+4.jpg 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEis-FhcgbpFqBIFBOBHW0e-UXbTAy-OzVwSG3xG0HTSNBDq41gJtoQ2H-VX4B_YRHSVV7sViBcqVjQ-8mDwcwbWMsK6n9AxCM5wyu9md5ryx56japrGburonbJxnwB87GZXtQBfKhnO66CW/s1600/MWAKYEMBE+2.jpg
Mhe. Mwakyembe katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo hicho.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhx4TDnJZZCyADBZ84hZImgFD6fNCIx7r-r7GUcVvJ4d4_EYzRKL7kPcJH89vcsTwSqmB3FfV6aFOXF9J0ZvRwZk0fs4mtY995ZQWO-eAUEvd0hqYSNPQInG2-d5ktANQzGyshzjBRJP4SW/s1600/MWAKYEMBE+5.jpgMhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, Bw.Suleiman Saleh Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Eng.K . Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga, Mkurugenzi wa Mradi (Terminal 3 Building), na Bw. Andrew Magombana katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya General Electric ya Erie, Pennsylvania.

Na Mwandishi wetu, Washington, DC

Mheshimiwa Dk.Harrison Mwakyembe(Mb.),Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya kikazi nchini Marekani katika miji ya Washington DC, Erie, Pennsylvania na Detroit, Michigan, kuanzia tarehe 18 -22 Septemba, 2013, kwa mwaliko wa Bw. Robert Shumake, Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jimbo la Michigan.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe.Mwakyembe ambaye alifuatana na Bw. Lupatu, Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji katika Wizara ya Uchukuzi, Eng. K. Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga,Mkurugenzi wa Mradi, Terminal Building 3, na Bw. Andrew Magombana, Msaidizi wa Waziri . Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC na kisha kusafiri hadi Erie,Pennsylvania, kufanya mazungumzo na uongozi wa Juu wa kampuni ya General Electric inayotengeneza injini za treni.

Katika mkutano wake huo Mhe.Mwakyembe na ujumbe wake ulipata fursa ya kuelezwa shughuli mbali mbali za kampuni hiyo pamoja na kutembelea karakana kuu ya kampuni hiyo yenye watumishi zaidi ya laki tatu. Akiwa mjini Erie, Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kueleza mikakati iliyopo ya kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania pamoja na kujenga mashirikiano zaidi baina ya kampuni na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha azma hiyo.

Baadae Mhe. Mwakyembe na ujumbe wake ulisafiri hadi katika mji wa Detroit,Michigan, ambapo alipokelewa na alifanya mazungumzo na Bw.Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye makazi yake katika mji wa Detroit.

Akiwa mjini humo Mhe. Mwakyembe alitembelea kituo cha mafunzo ya Urubani ambapo alielezwa historia ya kituo hicho pamoja namna ambayo kituo hicho kitasadia katika kuanzisha kituo cha Mafunzo ya Urubani nchini Tanzania.

Aidha Mhe.Mwakyembe alipata wasaa wa kuonyeshwa aina ya ndege mbali zinazotumika katika mafunzo hayo. Kituo hicho kimetoa mafunzo mafunzo kwa marubani 3500 tangu kianzishwe miaka kumi na nane iliyopita.


WAZIRI MEMBE AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 23, 2013 | 2:34 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLZiDXuMVnWFb5DzLA8c1e714NfgNRx_XL4lYX57yjaZJxEp4c7NxPyHOv9fNYGPW8bHOXdJaT2f6cb8vR0QeZz1dNff6YFE0msEU24Ncc8_hzdtFywNezIedjegS5AiSgBCsGMzleiu0/s1600/DSC_0136.JPG

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimsikiliza  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Kamalesh Sharma walipokutana mjini New York kwa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya hiyo, ikiwemo maandalizi ya Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali (CHOGM)  unaotarajiwa kufanyika nchini Sri Lanka mwezi Novemba, 2013. Mhe. Membe yupo mjini New York kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68  cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Picha na Rosemary Malale

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvO9va5ZEwfEVmSGa6nw_kWlLahjamWNuq0UBCun5sXCXa6jPMpIeJjOlo07ahKIrJDxS_hNQbmsh55MiOnNnryFxlbmgDI503ohx-tyUtlHrwGypKEMOm3AObNsMY2oNHYzb4iE5a1yQT/s1600/P9224020.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo kufyatua matofali na vijana wa CCM walioweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Mji mdogo wa laela tarehe 22 Septemba 2013. Lengo kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera za Chama cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa ujumla. Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWEXAeRzcBYQykkDncA-XN5ye7aLRbhYenPLf8c15eGANTvLhwuSxDHl3dYbBRfBvImRfTxPKKxuplep5eJXCzp4d_3eQOv_ctOODQ3R2_jiWaWv0Dxt0d-J7oSDO4WLf4sxeKv3j6InTC/s1600/P9224034.jpgMkuu wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma akiwahamsisha vijana hao kukipenda chama chao kwa kuweka uzalendo mbele katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Chama hicho katika mji mdogo wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka kushoto ni Matin Matete Mjumbe wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa, Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Persin Kalikule Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhOBUpllUApY1IL0cSpQCtfWrzL1nAYAL3ZVz7jC3YMM2fmfK8LASbcMSE5ezNb_HaTV7veZBnAV8B-_4IwWOrY6DQjLyaCjei8F8YvsZej5Z_A9uH0GaPna_TpN5VAEWeAGZrt9Qb6YOX/s1600/P9224027.jpgSehemu ya vijana hao waliotoka katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakionekana kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo iliyopo katika mji mdgo wa Laela.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj73JIyYcwR-UD7hLPmUqmKGRowr68BxkhVX3FGuIZ995RewxsmnhDqVIsQbG-52obV2Lqu7opohXxxOXZt7qLM_krbxlvJLmOCpKj6uqHycD6pXu2zBZJ8sRdI3VhtJiSdMKzK9Vm7h0Bv/s1600/P9224031.jpgMwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao  akielezea mipango mbalimbali ya umoja huo ikiwemo uhamasishaji na upandaji miti ya mbao kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi Mkoani Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtDTBkF8ir5H-ntT5xWCfdiaCBk6xe_0rC5WxveRN6SNxGgZA_Xvhdppqv1B52fvEp6DRkqEvbHpWEM75VGvbZxPEcaGPFxKFeYKb4Dqkyi7M55Mi7BnnIt_cbKhb3m9VCIlYxfotr3cgf/s1600/P9224044.jpgMkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na viriba vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM Mkoa wa Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la upandaji miti wa kibiashara.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.)

WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, September 21, 2013 | 3:18 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrrBf8sYp0C2yw21-IGAdn9JwRba1K3Ll0CaB20mY1wSNqV11WncCjANHXkVWkp6_UnQ3XKnj1XjxkW4T4wTBCKeVPJYmOqHrbpXU1wC4z7Tr7tc6vELooJYZ_cQ3wDcchOy-Gcm3GTIN1/s1600/PIX+1+(1).JPG
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZvw2omjgLjZKn1MAUkg7RuXxRL8lVCnpaWIeaTHbC3hXa7ptZfCOgPJrpw41An6ksfjFjMgNUM5KVaR-0wgRgRAfjwWkm1kzKnt9_IvAs0Opu-tHuYDxCE_Nerd556_955wjdlWx0Nh6K/s1600/PIX+2+(1).JPG
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Mjini Unguja, Zanzibar alipofika katika Hospitali ya Muhimbili kumpa pole, ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCubOnNoXElJ23awFKbbczeEcTlLWpWYNk_K693yQ1wON9tHhYO7-VlzeRm183nov90YBSArz2xX5GGvmBrSid60ED3_va6IHfgP79ASGukuNo1oMUHPL-n8h0LjOEPvnA-nSbFcoNj6Ew/s1600/PIX+3.JPG
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimuhakikishia Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar jinsi wizara yake itakavyopambana kwa kuwakamata wale wote watakaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali. 

Dk Nchimbi alifika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole padri huyo ambaye anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi. Hata hivyo, Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.

Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


MKANDARASI WA BARABARA YA MBEYA HADI LWANJILO KUILIPA SERIKALI SHILINGI BILIONI 16

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbYBfICSFb5GlhZ53f-99wTpApq-kqxcj-9GUpU4cM6_TE4P7fzvAnQ2PhPvZ7au_GePXsjsQy8j2boIvRB7e7Q9ItS_C4YNgk2Uzi6kLO6XDf3mcxvUTa6Gqj9DoE2Lle5t6Mz1vCxXYu/s1600/Picha+1.jpg
Mhandisi Mkazi Eng. Peter Gibson (aliyenyoosha mkoano) kutoka Kampuni ya Nicholas O’ Dwyer & Partner akimpatia maelezo Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli, kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara ya Mbeya – Chunya. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJRTplTb-AYn9pcO-DH9q4nUc-hXAmDhTOqSCXA_YtR36IB3lksyI5Az5TufgR8hgYCd6Q-p1QvKJnGtW0uTHjOu_Q6EF1nuvpleErydZ3QbpVdOHaFyCNtp3RPWQkvIj6IOwUEGyWECUI/s1600/Picha+2.jpg
Waziri Wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli (katikati aliyeinama) akiangalia mamendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mbeya - Chunya. Kushoto kwa Waziri Magufuli ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgxOHFj7YJXt6_2a4tGEJuuIZ1s41XSTxmQdH2mpYFyieQNyb33gukVVjNBu39c-5Nh3jSYPyUcrdHmLnGp2ggfKqb67mNhiiXF098Z1R0veRd6FiEh-FkIU4g6unxHbzbVRE09oKLk1-po/s1600/Picha+3.jpg
Waziri Wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli (aliyetangulia) akikagua mamendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mbeya - Chunya. Nyuma ya Waziri Magufuli ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandolo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj08TStTWYmkTHpORmGBfuXZs4zDsSp-GTHYyOQfF0tUQHGe5QAVEc85mjSFUCsqV5qAiVNSnpFRjmx0w8Oy3aqa39o5VRWg3S-vf1_VcppSer-tB5jZUMZegc3X-74vUFFFN4GcQJaI0m3/s1600/Picha+4+(1).jpg
Mhandisi Mkazi Eng. Peter Gibson (kushoto) kutoka Kampuni ya Nicholas O’ Dwyer & Partner akimpatia maelezo Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli, kuhusu uwekaji wa lami katika barabara ya Mbeya – Chunya sehemu kati ya Lwanjilo na Chunya.


Mkandarasi aliyekuwa amepewa kazi ya kujenga barabara ya kuanzia Mbeya mjini hadi Lwanjilo kwa kiwango cha lami anatakiwa kuilipa Serikali ya Tanzania Shilingi bilioni 16 baada ya kushindwa kesi. Kampuni ya Kundan Singh ya kutoka Kenya iliachakazi za ujenzi kinyume na mkataba na kukimbilia mahakamani ambako imeshindwa na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Wananchi wa Chunya walijulishwa uamuzi huo na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiongea katika mkutano wa hadhara mjini Chunya. “Baada ya mradi huu kusimama kwa muda mrefu kusubiri maamuzi ya mahakama hatimaye mradi huu sasa unaendelea na mkandarasi aliyetupeleka mahakamani ameadhibiwa kutulipa shilingi bilioni 16” alibainisha Mheshimiwa Magufuli.

Wizara ya Ujenzi inaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kati ya mji wa Mbeya na Chunya kupitia Lwanjilo. Mradi huu umegawanywa katika sehemu mbili ukianzia Mbeya mjini hadi Lwanjilo yenye urefu wa kilometa 36 na sehemu ya pili inaanzia Lwanjilo hadi Chunya pia ikiwa na 
urefu wa kilometa 36.

Mheshimiwa Magufuli aliendelea kufafanua kuwa tayari kuanzia mwezi Desemba 2010, mkandarasi mpya alikwishapatikana na atakamilisha kazi ambazo ziliachwa na mkandarasi wa awali ambaye aliingia mkataba mwaka 2007 na kisimamisha kazi mwaka 2009. Kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC) imeshinda zabuni ya kumalizia ujenzi wa sehemu hii ya kwanza kutoka Mbeya mjini hadi Lwanjilo kwa gharama ya Shilingi bilioni 55.4. Mkandarasi huyu baada ya kuwa ameongezewa muda kutokana na mabadiliko ya viwango vya kazi sasa anatakiwa awe amekamilisha mradi huu 
kabla ya mwezi Desemba 2014.

Akizungumzia sehemu ya pili ya mradi huo ambayo inaanzia eneo la Lwanjilo hadi Chunya, inayojengwa na Kampuni hiyo hiyo ya China Communication Construction Company (CCCC), Mheshimiwa Magufuli alimtaka mkandarasi kuwa amekamilisha kazi zote ifikapo mwezi Aprili mwaka 2014 kama mkataba unavyomuelekeza. Sehemu hii inajengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 40.2.

Kuchelewa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara kati ya Mbeya na Chunya kumekuwa kukilalamikiwa kwa kipindi kirefu. Hivyo kupatikana kwa mkandarasi wa kumalizia kazi kwa sehemu ya kwanza kumeleta faraja kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao waliitikia vyema wito wa kubomoa majengo yao yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi mradi huo.

Mh. Wasira azungumza na watumishi Mkoani Lindi

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, September 20, 2013 | 9:27 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaphmLxHbjOZNLlnO6jHy1d2eB5jHdg9Gg6xDS63O105rpf_eJXW1I8wM1YUsS0O7pI4ZMMCChJp8JfQLmzVMOE07Eq_XlaVJBuPdewQut5_gIIuilcCI7a8AXzYAiNs_pvoumvKr9CoD7/s1600/IMG_3937.JPG
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen Wasira (aliesimama) akizungumza na watumishi mkoani Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi. Na Abdulaziz Video,Lindi
 

WATUMISHI wa Serikali wakiwemo wataalamu mbalimbali,wametakiwa kuwatumikia wananchi,wakiwemo wakulima wa zao la korosho kwa kuwawekea Mfumo ambao utawapa Haki itokanayo na jasho lao.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen Wasira,ametoa kauli hiyo,alipokuwa akizungumza na watumishi mkoani Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi.

Akizungumza na watumishi hao,Wasira amesema Serikali inajipanga kufanya marekebisho ya ununuzi wa zao la korosho kwa kutumia Mfumo wa Stakabadhi mazao Ghalani,ili kumuwezesha mkulima kulipwa fedha kwa lengo la kunufaika na Jasho lake.

Wasira amesema iwapo hakutakuwa na mfumo mzuri wa kuwatendea Haki wakulima hao,ikiwemo kuwasimamia vizuri na kuwalipa fedha zao, itakuwa ni vigumu kwao kuondokana na hali ya umasikini unaowakabiri hivi sasa ndani ya Taifa lao.

Amesema iwapo watumishi ambao watashindwa kuwajibika ipasavyo kwenye maeneo yao ya kazi,hakuna sababu ya kuwapandisha vyeo au kuendelea kuwepo kazini.

“Hivi mtumishi mfano Afisa Kilimo ameshindwa kumbadilisha mkulima kutoka kilimo cha kizamani na kwenda cha kisasa,kuna muhimu gani wa kumpandisha cheo,,,,,,,,hapo asilalame kwa nini hajapandishwa Cheo licha ya kuwepo kazini kwa muda mrefu,hapo anatakiwa aseme kwa nini anaendelea kuwepo kazini bila ya kufukuzwa”Alisema Wasira.

Waziri huyo wan chi Ofisi ya Rais,Mahusiano na uratibu,amesema kamwe umasikini wa wananchi wakiwemo na wakulima hautaweza kuondolewa kwa utaraibu wa kuwaibia mazao yao,kwani kwa kufanya hivyo bado wataendelea kujengewa mazingira magumu ya maisha yao

Hon January Makamba presents a prize to the over all winner of 2013 Young Scientists Tanzania

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFuyJwgsEGU6gb-GAjy_itZP6_MVpiXfNMEaN4FfX77GD707Ha0bkmHm93i9IQHp2yqk1TPbJx6mBW9od91DX1uip0vgxy3MlGnFzJ9tUoOCPB7l8Tge-NuNWsVkLWOM8JFq6NvMiKmHhM/s1600/New+Picture+(20).png
Deputy Minister for Communication,Science and Technology Hon January Makamba(right) presents a prize to the over all winner of 2013 Young Scientists Tanzania Jafar Ndagula and Jeremiah Vincent from Singida.Looking on is an Irish Ambassador to Tanzania her Excellency Fionnuala Gilsenan.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDgQ2MeeBBp56HY_MbEpP5vvTv6DJayd8ZaR0H1HZOy1VbvDVMCmfaeVpBUjay5YnB-5d29hu0D0sDKBJEHN2hoh0qFPYTfrWUnJzJVftFjPysgLh1omYx1LJJ2IA5KmVH2tqdWIkjx6Mh/s1600/New+Picture+(25).png 
The over all winner of this Year’s Young Scientists Tanzania 2013 Jafar Ndagula and Jeremiah Vincent from Singida (left) about to take their prize from the Deputy Minister of Communication,Science and Technology Hon January Makamba.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaFQVQwJ7c0-dzMLrkNCtzwrAewkID60vmW5jK4VN6F6IHeA9YTZ6boGLaqiiQDyMl_JS8YJbXDfk-RDCU7v_sD6AZaOjFXoAnNfc1jRvfyFMNOUjCwK_CmnPzCV74l2OTG8CjW2gofY0g/s1600/New+Picture+(26).pngSecond runner up winners Shemsa Abdulkarim and Salha Said(left) from Haile Selaisse Secondary School of Zanzibar receive their prize from the Deputy Minister of Communication,Science and Technology Hon January Makamba and the Irish Ambassador to Tanzania her Excellency Fionnuala Gilsenan.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhG77bAEFM-7YISqx9PFaYIgwrVej0jjxJYDtTXfQ0ItHmhHHaDsBzEfCAYjW3sx81hm7-wjQt-mN70EXQMnfgPxajJIdWDLKZUN0v17mo5wKWkKupzNbkvJ-9fQ-9HpgQXBRxHJKNzj5SQ/s1600/New+Picture+(23).pngSecond runner up winners Shemsa Abdulkarim and Salha Said from Haile Selaisse Secondary School of Zanzibar show their awards.Apart from the trophy and a One Million Tanzania Shilllings,the Young Scientists will also have a chance to travel to Ireland to explore more scientific innovations.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKY7MjrTRBdX2M5ItV4c-GsT9KCOEaB6tocrEcXo0QFPepkyIYWtIVAGfGQDIaxVjj3D4AFe9XN3SjTKKbWb7QDMAylGlKrMPZjHLEOdg1QiVEzXeEt8dHxcgxVSqI4iPOdrl7lUl2s_yG/s1600/New+Picture+(24).pngThe Deputy Minister for Communication,Science and Technology Hon January Makamba looks at a Drip Irrigation System Project which uses recycled materials shortly before announcing it the over all winner of 2013 Young Scientists Tanzania .The project has been developed by the Singida boys,Jafar Ndagula and Jeremiah Vincent.

UJENZI NA UKARABATI WA BARABARA YA BUNDA MPAKA MUSOMA MKOANI MARA UKIENDELEA LEO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmMCeHC9s1qdVhJ72ugu6VJ0vzErYxQI0WfCW8XYUiarlm47PkyGuwgpt7WiNMCqr32ybJZsHizoUvWyr8mogB91ekFbrnjCQGvtvcEon-mSvJB7IQs5MgOgXJdsjg9dJTDraqsdPDp8ZT/s1600/3.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAT7GEKFEGT0pwhCmlBTE0ws7QwLr1gyQ_WygkBdPfaxeM55_CkxGZb0zOwiM1ZjFSr8DxmC7PSykxaC9AD8clIvPUGIT_1mms9Wjffft0Vo8068jLaRQ32uHj9zA5NvzcfmPBE2vYh4KH/s1600/4.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimQzEgqpZ1tV59yUxu7TOM9KkctB53blX4wy_S-Uxh7uyiIal8C_GrsNPSOkGexposRpumRCW7q8swqycX_8F1nHqn3kETgOCtYkyZ21zciLhaA64K0o2C0JbiuxL7MpAwmCY5yop2zQih/s1600/5.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3eQY9qesvylL9RxVAgOOC00ABTtu8LO2alNFtlxLzGAyNDECqoNBsEIpV3sdBZe66SuhgG_gCkZ4519rN5405cmoh6CtNXAzZClPZk-rEaHrJqc2O3l3uD4wzjJOqV4S2y92_aCbqdZAO/s1600/6.jpg

MHE. LUKUVI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI CHA DEW DROP KILICHOPO SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEir2cmsU-Cx87Xi04HzuRJdeQwwbJQKd0ENdgTeYrtI0IudgLfV8ZaHkr-7jak9Oi-XrPuwW8IxdAfaI7rcFp0eQmnKbOv3ft0V_ay-8oJlhk2l67ac2jxwTIMI0lz1ggMiLmW7d9XxwnXD/s1600/P9183968.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akikagua kiwanda cha maji cha Dew Drop kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani Ndugu Aziz Tawaqal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa tarehe 18 Sept 2013. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCS4PEFfeSZ0td3zcSKnThvXxlz4Lw8blL6HF35OEhqabRqKdI_Lwx08j_eijzGO-lqje-FCGXC33HoCgqd_ORgs2Px2G7nQD9c2Jf990D7DXiU9AF2PBSts4qSDkWfLx4pGQPEUMKUh9_/s1600/P9183975.jpg
Kiwanda cha kisasa cha Dew Drop chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa saa yakiwa na ubora wa hali ya juu. Maji hayo huzalishwa katika hali ya usafi na hayaongezwi  kemikali yeyote ambapo husafishwa kupitia "Sand Filters", "Activated Coal" na teknolojia ya "UV Light".

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCyaa7bw4ZcjfM3hZiSrXG6q9hz6B9eUI5dClJMEjm1zDkxl75t_Mu2Y72UYGhl_FMFCovGwOJnxkL0fse6FuwFEcIx5WNwYXbF7wUbF9zAwecdrlpjGq4NfR6SK0fELSQXsabARnyOdsu/s1600/P9183969.jpg
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi alipofika kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za muwekezaji huyo ikiwemo kiwanda cha unga cha Energy Milling. 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzW8da9Ol1-oZg1mqO0VWWNbL2SKmhwhzmEB_7JnWOEVNQehsVECthOKm8sRI6Dyphd2nVZkiQmdz7S4KsXNRGdU8XmWclmI1TRGKB1gwLE4CB4Pp2jJ144M1wFWm-n764b0jfkxeg59V3/s1600/P9183977.jpg
Waziri Lukuvi akipokea maelezo ya Maji ya Dew Drop kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal, Waziri huyo aliyasifia maji hayo na kusema kuwa ameyanywa na ni mazuri sana ukilinganisha na maji mengine yanayozalishwa hapa nchini.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa...rukwareview.blogspot.com)

Mhe Ndugai na Balozi Kamala waongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Nchi za Afrika,Caribbean,Pacific na Jumuiya ya Ulaya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiny0BErvRGioQANar62LV88QXiGFqKXozC-qzjsaVeFeBMUD7XZBvKScYob5T63qnra4_grZzy4WB73R040Fno5U8b1gkLA8C31Vt4um9sU6flYU0wY8dOr2UmLIooppWsV5ERRUUGC_64/s1600/2013919181246.jpg
Mhe Job Ndugai,Naibu Spika wa Bunge akiongoza kikao cha pamoja baina ya Wabunge wa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific na Wabunge wa Jumuiya ya Ulaya kujadili masuala ya kijamii na mazingira.Mhe Ndugai ni Mwenyekiti Mwenza(Co Chair) ambapo mwenzake in Bi.Michelle Rivalsi (pili kushoto).Mkutano huo ulifanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya jijini Brussels.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhkPav4n53Nx5NKN56VmzcAKyrQ-KSawX1DbXmyBeMhaaWSRZI_nk3GSq_21oB7v-ZQ64vnrzQwykX9rNm0EvMDepF4OB9tKDURKBcLlNXVSHxSmkvpoWcpFeRGcszhOPtXYDjcXzK8VO3/s1600/2013919181129+(1).jpg
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mhe.Deodorus Kamala (watatu kushoto)akishiriki mkutano huo pamoja na ujumbe wa Tanzania unaowajumuisha Mhe.Mussa Zungu (wa pili kushoto),Mhe.Dr Mary Mwanjelwa (kushoto) na Bw.Aggrey Nzowa ambae ni Katibu wa Msafara huo na pia Mkurugenzi Msaidizi (Huduma za Maktaba) katika Ofisi ya Bunge. Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger