Home »
Label 5
» WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA
WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA
Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine alioambatana nao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,
leo ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya,
kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi
lililotokea Tarehe 21 Septemba 2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi
sasa zaidi ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179
wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika
hospitali za Aga Khan University Hospital, Hospitali ya Nairobi (
Nairobi Hospital), na Hospitali ya MP Shah.
Katika tukio hilo pia
Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection,
UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa
kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana
Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea
kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment