Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira.
Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema.
Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.
Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu.
Alisema hoja kuwa ambayo imewakera na kuwasumbua Chadema ni hatua zinazochukuliwa hivi sasa kwa pamoja kati ya Serikali ya CCM na Serikali ya China ambayo hivi sasa inaelekea kuzaa matunda ya kutoa mwanya wa ajira zaidi ya elfu- 25 viwandani.
"Tayari tushaingia makubaliano na serikali ya China ya kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani ya mazao kama Pamba, ufuta, alzeti na mazao ya mifugo ikiwemo ngozi za ng'ombe, hivyo wananchi, chuki na hasira ya Chadema dhidi ya Balozi wq China inasababishwa na mafanikio hayo ya kutatua matatizo ya wananchi" alisema Nape.
"ushahidi wa hasira za Chadema unadhihilishwa na ukweli kwamba tayari wawekezaji wa viwanda hivyo vya kuongeza thamani ya mazao washawasili nchini na wengine wameshaanza ujenzi wa viwanda hivyo mjini Shinyanga, na kwamba vitaanza kazi ya uzalishaji mwezi desemba mwaka huu" Aliongeza.
Nape aliwataka watanzania kuzipuuza shutuma za Chadema dhidi ya Balozi wa China na kusisitiza kuwa hasira yao imesababishwa na hofu ya mtaji wao wa kutumia udhaifu na umasikini wa watanzania hasa vijana wasi na ajira kama mtaji wao wa kisiasa.
"Chadema wamechanganyikiwa, kwa sababu siku zote wamekuwa wakitegemea kuendesha chama chao kwa mgongo wa umaskini wa watanzania, sasa kasi ya kutengeneza ajira kupitia ujenzi wa viwanda, na mchakato wa kuwezesha kuongeza bei ya mazao ili kuwakwamua wakulima kutoka katika umaskini umewachanganya" Alisisitiza Nape.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Balozi wa China alishiriki katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdurlahaman Kinana kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa viwanda vinavyojengwa na wawekezaji toka nchini China katika mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo vile vinavyojengwa mjini Shinyanga jambo linalolalamikiwa na Chadema.
0 comments:
Post a Comment