Rais Dkt Jakaya Kikwete akitembea kwa miguu kutoka hotelini kwake kuja kwenye Ubalozi wa Tanzania Marekani siku ya Jumatano Sept 18, 2013 na kukutana na Mabaozi wa Heshima ambao jana Jumatano wasaini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataofanyakazi za kuitangaza Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya uwekezaji, Utalii na mambo mengine yatakayosaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
RaIs Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama William alipokua akiingia chumba cha mikutano cha Nyerere.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea machache kuwashukuru Mabalozi wa Heshima kwa kukubali kwao kuitangaza Tanzania nchini Marekani na kusema sio kazi rahisi lakini ana Imani nao na aliwatakia kila la kheri ya kuwa na nia thabiti ya kuitangaza Tanzania nchini Marekani.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake kutoka Michigan. Kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula.
0 comments:
Post a Comment