VINGINEVYO CCM ITACHUKUA HATUA KALI DHIDI YA WATENDAJI WA WIZARA HIYO
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia waimbaji wa kwaya mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nyashimo Wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu, Ndugu Abdulrahman Kinana amemaliza ziara yake kwenye mkoa huo ambapo amekagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wenyeviti wa mashina pamoja na wanachama wa CCM ili kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali moani humo, Kinana anaaza Ziara ya siku sita katika mkoa wa Mara.Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus Kamani.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo uliofanyika mjini Lamadi Busega Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa,Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasia pamoja na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili kumaliza tatizo la malimbikizo hayo,
Kinana amesema kama watendaji hao wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya Kikwete
ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu,
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakifurahia ngoma za akina mama walipowasili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha bodaboda wa Nyashimo Gasper Mabula
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimnawisha mikono Mwenyekiti wa shina Sina namba 1 kijiji cha cha Nyamatembe Bi. Sophia Kayenze tayari kwa kupata kifungua kinywa chachai kwa Michembe .
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika kijiji cha Nyamatembe.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumza na wananyamitembe mara baada ya kuwasili kijijini hapo wakitokea Bariadi.
0 comments:
Post a Comment