Omari Kimweri
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia amendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo
Bondia huyo ambaye anaitangaza vema nchi ya Tanzania Kimataifa ameaidi kuwa ataenderea kutoa vipigo kwa mabondia mbalimbali pindi wakutanapo ulingoni
Bondia huyo aliezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo uku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye uzito wa light flyweight
Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman Gonzalez na IBF light flyweight title unaoshikiliwa na John Riel Casimero wa Philippines ambao wananiumiza kichwa kwa sasa kwani ngumi ulimwengu mzima ni zile zile ila tunazidiana maarifa
Bondia huyo anaefanya shughuli zake za masumbwi nchini Australia ana mpango wa kuja kuwekeza nchini Tanzania mchezo wa masumbwi ili ukuwe hapa ambapo atafanya kila jitiadi ili mchezo wa masumbwi uweze kusonga mbele nchini habari hizi kwa ushirikiano mkubwa wa mtandao
0 comments:
Post a Comment