Sema Naye: Label 3
Headlines News :

NEWS

Latest Post

Showing posts with label Label 3. Show all posts
Showing posts with label Label 3. Show all posts

ASKARI WA JWTZ ALIYEJERUHIWA CONGO NA KUFARIKI AAGWA LUGALO, DAR ES SALAAM

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, September 24, 2013 | 3:07 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9yy3zmnIlAI-ZL_WAYdINyFKqmAxcwA8kk6KLCUR8BgT6Xq_-JV59tFJ9uh8cDKeZwyDwgH-c_KDS7Ns8v6Jr92LYeg0FDvlQixq6cYLZuxKLz2C5xQjU8LeYZkG7dhE410Ud5Athh5ac/s1600/JWTZ.jpg
Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Askari mwenzao, Marehemu Private Hugo Munga alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu huko Pretoria Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa na vikosi vya MONUSCO Congo DRC katika operations ya kuwaondoa waasi wa M23. Mwili wa Munga ulisafirishwa jana kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika Viwanja vya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJQ2eg2udi7pHjuT3duh4MpFvFy_qjjb6vKGhWxZ5hxlaePr2Wx5li6DhOBCT1UehJHOEhBiAMwu0sLmirxcoyiohhOHbYGMmUbyPo3QNigTxWMS5Isu3Wb54ONYOdHNtW6Op7He1uL2i-/s1600/MAMA+1.jpgMama wa Marehemu, Jovitha Barnaba Munga akisaidiwa kuaga mwili wa mwanae.
 

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdzS79BAhqc8RJkiHVLNlft_ox5-FxT5xWTapT2bVNiBBnPuVdo7pj6-GqeISH7HEQJgntPRY2RJS7pEPLPvMKz_2CJIXdng7z1gSTWifX68oQXnomhO-1COxiesa8cyaOHerjnXz5ijcd/s1600/IMG_1553.JPG 

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi11BizhOawL93HZhBqHRIry0e0m4hg9V5WEJo6dxIX8AG0kg2wx63m9m2idBTh3rQBUiiFgJzZ6rzMGMc9vbkcB7KTw1MEkMxHYaYcKObIW8Ml9A37eYhCiCeG_8jLkl19xaKhRrNNDWFA/s1600/IMG_1522.JPG
Baadhi ya waombolezaji ambao ni Askari wenzake marehemu pamoja na wana familia wakiwa eneo la tukio.Picha Kwa hisani ya Father Kidevu Blog

Mh. Lowassa aongoza Kikao cha Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden leo

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, September 21, 2013 | 3:23 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWsIOTjlP-dpbYKDZHI2xMjZrrOc3VBAoBM_S4C4M-rL5zakC1o2DIFwJT9JJPS2gSER9cIB_evHUWFMYqpLpDNHd3R_f-VnkJuCoxmy_njUCh1As6Xqbo0hBF0GSOEEk4bXzmNmilD8mS/s1600/photo.JPG

Mwenyekiti wa Kamati ya BUNGE, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Edward Lowassa akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa kikao alichokiongoza wakati alipokutana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Stockholm,Sweeden.Waliohudhuria kwenye kikao hicho ni Balozi Muhammed Mzale,Mhe. Juma Nkamia,Mhe. Suzanne Lyimo,Bw. Jacob Msekwa,Bw. Athuman Brambath,Bw. Yusuf Mndolwa,Bw. Arthur Mwambene na Bi Apronia Rutaihwa.Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi huo.

Balozi seif ali iddi akagua hoteli zilizoungua moto kijiji cha Kendwa, Nungwi, zanzibar

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 8, 2013 | 5:13 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiB7QxxFfEct-ZykDcMg6rDSyx2vre6SpS2iiYFAKKoBNT1n4tiirF75gqS_k8IEUjm6nVF7-Hhv21IF-Q69OYExDIuIah-p7XCvY6ONUN_7ijWqkS4rTeG1Cf02KBb8ZdqjyfbjsKf5wMt/s1600/627.jpg
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set Bungalows iliyoko katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Abdullsamab Ahed Said akikagua athari iliyosababishwa na moto mkubwa uliyoyakumba baadhi ya majengo ya Hoteli hiyo juzi jioni. Pembeni yao aliyevaa kofia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” Machano Fadhil Machano { Babla }  na Nyuma yao aliyevaa suti za Bahari ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiilVOCDF0G9WpCcCbSK4YXuRXfuNbo7NV1CAdXBgy1Y7aoKSr3tjljCEGUJno_-Qfa3Hkv4tesiTJ17Pp_Iehbsmwsk8F1an6fbI_cQpktK8vooriFOhAPEgfzjeIq4CpJxiGPJBro-7W6/s1600/647.jpg 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  Pembe Juma Khamis akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hali halisi ya moto ulivyoikumba  Hoteli ya White Sand iliyoko Kendwa Nungwi Mkoani humo juzi jioni.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgu_cI9C4dhR6aDHlIR2juGkKMMR_OgI5A1edVVsRjteGspmDKvXqOrlXfSybZrqiZ_C9BEH9Ltd9thx3MvSIhG3QHIGyul8N72M0dldIJNYYu9kLKZxz9KUaPR66tj9eUleGXBcd8UJkle/s1600/655.jpg 
Baadhi ya Majengo ya Hoteli ya White Sand iliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Kendwa Nungwi ikiwa ni miongoni mwa majengo 10 ya hoteli hiyo yaliyoteketea kwa moto mapaa yake juzi jioni.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

-----------------------------------------------

Hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja Nukta 2 imepatikana kufuatia kuungua kwa moto hoteli mbili za Kitalii za  White Sand na Sun Set Bungalows ziliopo katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Wilaya ya Kaskazini “ A” Mkoa wa Kaskazini Unguja juzi majira ya saa 11.00 za jioni.

Hoteli ya Sun Set Bungalows inakadiriwa kupata hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 400 wakati ile ya White Sand  iliyoungua zaidi kutokana na moto huo inakadiriwa hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 800.

Moto huo ulisababishwa na hitilafu za umeme katika moja ya majengo ya Hoteli ya Sun Set Bungalows iliyoezekwa makuti na kutoa cheche za moto zilizosambaa kwa haraka katika baadhi ya  majengo mengine kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma katika eneo hilo.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akitokea Bungeni Mjini Dodoma alifika eneo hilo la tokeo ili kuwafariji Wamiliki, Wafanyakazi wa Hoteli hizo pamoja na Wananachi wanaozizunguuka Hoteli hizo kutokana na maafa hayo makubwa kwa uchumi wa Taifa.

Akitoa ufafanuzi wa  mkasa halizi wa tukio hilo  Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set Bungalows Abdullsamad Ahmed Said alimueleza Balozi Seif kwamba Moto huo umevikumba vyumba Vinane vya  kulala wageni, Stoo pamoja na jiko la kupikia.

Abdullsamad alisema Wageni wapatao sabini waliokuwemo kwenye vyumba vya Hoteli hiyo waliweza kuokolewa kwa ushirikiano kati ya Wafanyakazi wa Hoteli hiyo na Wananchi walioizunguka Hoteli hiyo jambo ambalo lilileta faraja kwa Uongozi pamoja na wafanyakazi wake.

Mmiliki huyo wa Hoteli ya Sun Set Bungalows aliwashukuru wananchi hao, Viongozi wa Serikali Wilaya na Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na Maafisa wa Kamisheni ya Utalii kwa msaada wao ulichangia kupunguza machungu ya janga hilo.

Balozi Seif Ali Iddi akikagua hali ya tukio  la moto huo ambao pia uliathiri Hoteli nyengine ya jirani ya White Sand ambapo Mmoja miongoni mwa  Viongozi wa Hoteli hiyo Ramadhan Msanif  alimfahamisha Balozi Seif kwamba  wakati wakijiandaa kutoa msaada kwa wenzao jirani wa Sun Set cheche za moto huo pia zikaanza kuvamia Hoteli yao na kulazimika kukabiliana nalo.

Bwana Msanif  alisema licha ya juhudi walizochukua kukabiliana na moto huo lakini kasi kubwa ya upepo uliokuwa ukivuma wakati huo ulisababisha kuathiri  mapaa ya nyumba  10  za hoteli hiyo katika kipindi kifupi kwa vile zilikuwa na mapaa ya makuti.

Akizungumza na Viongozi, Wafanyakazi wa Hoteli hizo pamoja na Wananchi wa jirani na Hoteli hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alitoa wito kwa wananchi kuendelea kusaidia wawekezaji wakati yanapotokea majanga kwenye maeneo ya vitega uchumi.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inasisitiza na kutegemea sekta ya Utalii ambayo kwa sasa inasaidia kuongeza mapato ya Taifa sambamba na kutoa ajira kwa wananachi wanaovizunguuka vitega uchumi hivyo.

Hata Hivyo Balozi Seif aliendelea kuwakumbusha wawekezaji vitega uchumi mbali mbali Nchini kujenga utamaduni wa kuiwekeza Bima Miradi yao ili wakati wanapopatwa na majanga au maafa Bima hizo ziweze kuwasaidia.

Alisema inasikitisha kuona ipo miradi ya kiwango kikubwa cha fedha inayoendelea kuwekezwa Nchini lakini wamiliki wengi wa miradi hiyo wanashinda kuikatia bima na hatiame inakufa kabisa pale inapokumbwa na majanga kama ya moto.

“ Wawekezaji na hata Wafanya biashara wengi  bado wamekuwa wazito kuiwekea Bima miradi yao na kusahau kwa kuona ghali  mpango huo ambao kumbe huwa unawasaidia wakati wanapopatwa na majanga “. Alifafanua Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi waliopo jirani na Hoteli hizo kwa juhudi kubwa waliyochukuwa na kusababisha  kupungua  kwa hasara kubwa iliyokuwa izikumbe hoteli hizo.

Alisema juhudi hizo zilizowaongezea nguvu za uokozi wafanyakazi wa hoteli hizo zimesaidia kuokoa mali na vifaa vya hoteli pamoja na wageni waliokuwa wakipata huduma ndani ya Hoteli hizo.

“ Nafarajika kusikia kwamba harakati za uokozi wa mali na vifaa katika Hoteli hizi mbili za White Sand na Sun Set Bungalows za Kendwa hakukuwa na ripoti za udokozi wa mali kama zilivyotokea Kwenye Hoteli ya Paradise Beach Resort iliyopo  Marumbi wakati ilipowaka moto wiki moja na nusu iliyopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Hoteli hizo kufikiria kubadilika  katika mfumo wa ujenzi wa mapaa ya makuti ili kujilinda na  majanga yanayoweza kuepukwa licha ya kwamba mfumo huo hutoa ajira kwa wananchi wanaouza makuti yao.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliangalia eneo lililopembezoni mwa Bara bara mbele ya Skuli ya Msingi na Sekondari ya Mto Pepo ambalo liko katika hali mbaya kimazingira.

Ziara hiyo ya ghafla ya Balozi Seif ilikuja kufutia baadhi ya wananchi kufanya Biashara katika eneo hilo linalotishia afya za Binaadamu kutokana na kutuwama kwa maji machafu yanayoweza kusababisha maradhi ya kuambukiza.

Katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuagiza Sheha wa Shehia ya Mto Pepo pamoja na Diwani wa Wadi ya eneo hilo kufika Ofisini kwake Vuga Jumatatu  ya Tarehe  9 Septemba  asubuhi kulijadili suala hilo.

Hali ya mazingira ya  eneo hilo mbali ya kutoa  sura mbaya kwa wapita njia na wageni lakini pia inaweza kusababisha mripuko wa maradhi  hasa kwa  wanafunzi wadogo wasiozingatia afya zao wa Skuli ya jirani na eneo hilo.

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AFANYA UZINDUZI WA MADARASA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI,ZANZIBAR LEO

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, September 7, 2013 | 1:42 PM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea Dagfhalia ya Wanafuzi wa Chuo hicho kabla ya kuzindua madarasa ya Chuo hicho leo huko Mbweni nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya kufundishia chuoni hapo alipofika kuzindua madarasa ya kusomea yaliyojenga kwa ufadhili wa Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake,baada ya kuyazindua rasmi madarasa ya chuo hicho leo ,hapo chuoni Mbweni,Mkoa wa Mjini Mgharabi Nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita,baada ya kuyazindua Rasmi madarasa ya Kusomea,yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,akitoa salamu zake wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,yaliyojengwa na Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,huko Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Afya Juma Duni Haji,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,(kulia).
Baadhi ya wananchi na viongozi walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

OPERESHENI YA KUWAVUA WAVAA "VICHUPI" MTAANI IMEANZA.., HUYU DADA AWA WA KWANZA..!!

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 2, 2013 | 6:36 AM



VIJANA wamechoka kuwaona wanawake wanaovaa kihasarahasara ‘vichupi’ mitaani ambapo wameanzisha oparesheni maalum ya kuwavua kabisa ili watembee utupu ijulikane moja.

Habari hii inathibitishwa na tukio la mrembo ‘miss’ (jina lake halikupatikana) ambaye amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbana na kasheshe zito kutoka kwa wanaume kufuatia kinguo kifupi alichokuwa amevaa, kilichoacha nje sehemu kubwa ya mapaja.

  JIJINI ARUSHA
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa ambalo lilishuhudiwa na shushushu wetu, lilijiri maeneo ya stendi ya mabasi madogo jijini Arusha, wiki iliyopita wakati mrembo huyo akiwa na marafiki zake watatu wakirandaranda kufanya ‘window shopping’. 


Mara baada ya kufika eneo hilo, miss huyo alijikuta akizungukwa na wapiga debe wa daladala na kuanza kumshushia maneno makali wakimwambia kuwa wamechoshwa kuona nyeti zao.

  AVULIWA
Huku sistaduu huyo akidhani ni kelele za kawaida, wapiga debe hao walimzingira na kuanza kumvua kigauni hicho cheusi.

APEWA KITENGE
Mrembo huyo alipoona mambo yameharibika huku wenzake wakitoka nduki, alilazimika kukimbilia katika duka moja la nguo maeneo hayo na kuomba msaada ambapo alisitiriwa kwa kupewa upande wa kitenge kwa msaada wa trafiki wa kike aliyemuokoa.


Kabla ya kusaidiwa na trafiki mwingine wa kiume, yule wa kike alimshauri kuvaa kitenge hicho na kuondoka eneo hilo.




AKIMBIZWA
Cha kushangaza, wakati anatoka katika duka hilo hali ilizidi kuwa tete baada ya midume walioonekana kuchoshwa na uvaaji wa nguo fupi kumkimbiza na kuanza kumvua kitenge hicho hivyo kusababisha vurugu kubwa kiasi cha matrafiki kadhaa kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao.

AJITETEA
Wakati dada huyo akihojiwa na matrafiki hao, alijitetea kuwa anawashangaa vijana hao kwa kumfanyia vurugu wakati nguo hiyo siyo fupi na mara nyingi amekuwa akiivaa na kutembea nayo maeneo kama hayo bila kupata tatizo lolote.


“Afande hii nguo huwa naivaa sana na sijawahi kupata matatizo yoyote, sijui leo imekuwaje lakini siyo fupi kama wanavyodai, nimevaa na kitenge lakini bado wananifanyia vurugu,” alilalamika dada huyo kwa uchungu.


Licha ya dada huyo kuwa katika mikono ya mmoja wa matrafiki wa kiume, jamaa hao walizidi kumfuatilia huku wakimrushia maneno makali ya matusi na wakati mwingine kumsukuma.


Baada ya trafiki huyo kuona hali inazidi kuwa mbaya, alisimamisha gari moja la serikali na kumuombea lifti kwa lengo la kumnusuru kufanyiwa kitu mbaya.

TUMEWACHOKA
Wakizungumza na gazeti hili juu ya tukio hilo, ‘machalii’ hao walisema kuwa wamechoshwa na uvaaji mbovu wa baadhi ya akina dada ambapo sasa wameamua kuwafanyia vurugu hizo mpaka hapo watakapoacha kuvaa hovyo.


“Tunakushukuru kwa kupiga picha, wanatuchosha hawa dada zetu, nguo wanazotuvalia barabarani ni za kuvaa nyumbani tena chumbani lakini wao wanavaa sehemu kama hizi, kuanzia sasa kazi itakuwa kama hii hadi watakapoacha, dawa yao ni kuwawashia moto,” alisema mmoja wa wapiga debe hao huku akisapotiwa na wenzake.


Siku za nyuma mchezo wa kuwavua nguo fupi wanawake ulisaidia kupunguza tabia ambapo kwa sasa imerejea kwa kasi hivyo ili wanusurike na adha hiyo ya kuvuliwa hadharani inayoshika kasi, inabidi kuvaa kiheshima

Stunning street performance in Rome - August 30, 2013.

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 1, 2013 | 11:17 PM

Stunning street performance in Rome
Street artists perform in downtown Rome August 30, 2013.[Photo/Agencies]
Stunning street performance in Rome
Street artists perform in downtown Rome August 30, 2013.[Photo/Agencies]
Stunning street performance in Rome
A street artist performs in downtown Rome August 30, 2013.[Photo/Agencies]
Stunning street performance in Rome
A street artist performs in downtown Rome August 30, 2013.[Photo/Agencies]

Tomato fight starts in Bunol, Spain

Tomato fight starts in Bunol, Spain
Revellers on a truck throw tomatoes into the crowd during the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
A reveller pours tomato pulp over another after the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
A reveller pours tomato pulp over another after the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
A reveller plays in tomato pulp after the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
Revellers pour tomato pulp over another after the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
A reveller lies in tomato pulp after the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]
Tomato fight starts in Bunol, Spain
Revellers battle with tomatoes during the annual "Tomatina" (tomato fight) in the Mediterranean village of Bunol, near Valencia August 28, 2013. [Photo/Agencies]


Rwandan troops heading towards Congo border, war looms

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, August 30, 2013 | 11:24 PM

 A trailer carrying a tank leaves the Rwandan capital Kigali en route to the border town of Gisenyi, August 30, 2013.
 A trailer carrying a tank leaves the Rwandan capital Kigali en route to the border town of Gisenyi, August 30, 2013.

Rwandan troops are heading towards the western border with the Democratic Republic of Congo, raising the prospect of another war in the Great Lakes region of Africa.

On Friday, a large number of people in the Rwandan capital Kigali watched a military convoy including troops, tanks and trucks loaded with artillery leaving for the border, The Associated Press reported.

According to reports, the Rwandan army troops are headed to Gisenyi, which borders the city of Goma in eastern Congo.

Congo’s adventurous neighbor is reportedly planning to launch a military offensive against a country with which it fought two wars in the past two decades.

Earlier in the day, Rwandan Minister of Foreign Affairs Louise Mushikiwabo said his country would defend its borders after rockets landed in Rwandan territory.

On Thursday, Rwanda accused the Congolese army, the FARDC, of firing bombs and rockets into its territory and said such "provocation" will not be tolerated.

However, the UN mission in Congo, known as MONUSCO, said late on Thursday that it had seen only M23 rebels firing artillery into Rwanda.

"MONUSCO has not witnessed any shelling by the FARDC into Rwanda. These are areas where FARDC are not present," said deputy UN peacekeeping chief Edmond Mulet.

Also on Thursday, the United Nations said that Rwandan military officers are fueling deadly violence in eastern Congo.

The UN said it had "consistent and credible reports" of Rwandan troops entering Congo to back M23 rebels.

The UN and Kinshasa have repeatedly accused Rwanda of helping the rebels in Congo. Rwanda has always denied the charges that it is backing the M23, but Kigali has never publicly condemned the militia, which occupied the city of Goma in eastern Congo for 10 days last November.

The M23 rebels and several other armed groups are active in the eastern Congo and are fighting for control of the country’s vast mineral resources, such as gold, the main tin ore cassiterite, and coltan (columbite-tantalite), which is used to make many electronic devices, including cell phones.

Since early May 2012, nearly three million people have fled their homes in the eastern Congo. About 2.5 million have resettled in Congo, but about 500,000 have crossed into neighboring Rwanda and Uganda.

Congo has faced numerous problems over the past few decades, such as grinding poverty, crumbling infrastructure, and a war in the east of the country that has dragged on since 1998 and left over 5.5 million people dead.

GJH/AB/MHB

Congolese army captures M23 rebel positions near Goma

 A Congolese army tank prepares to deploy for fighting against M23 rebels near the eastern city of Goma on August 23, 2013.
 A Congolese army tank prepares to deploy for fighting against M23 rebels near the eastern city of Goma on August 23, 2013.

The Congolese army has captured strategic hills overlooking the city of Goma in the east of the Democratic Republic of Congo after M23 rebels pulled out from the area.

"They did not leave by choice, they were confronted with the power of the army," Congolese spokesman Lt. Colonel Olivier Hamuli said on Friday.

The Congolese army, backed by new United Nations intervention brigade, has been shelling M23 rebels near Goma for some days to drive them back.

The Intervention Brigade has been given a stronger mandate by the UN Security Council to launch offensive operations against armed groups in eastern Congo.

"We won!" the army soldiers chanted in Kibati, until Thursday a rebel outpost on the frontline overlooking Goma.

The M23 rebels, who have been fighting against the army since April last year, said they withdrew from the Kibati hills to allow an independent probe into shelling that has killed several civilians in Goma and in the town of Gisenyi in neighboring Rwanda.

On Thursday, Rwanda accused the Congolese army, the FARDC, of shelling into its territory and said such "provocation" will not be tolerated, raising fears that Congo’s adventurous neighbor might launch a military offensive against a country with which it fought two wars in the past two decades.

However, the UN mission in Congo, known as MONUSCO, said late on Thursday that it had seen only M23 rebels firing artillery into Rwanda.

"MONUSCO has not witnessed any shelling by the FARDC into Rwanda. These are areas where FARDC are not present," said deputy UN peacekeeping chief Edmond Mulet.

The M23 rebels defected from the Congolese army in April 2012 in protest over alleged mistreatment in the army.

The M23 rebels and several other armed groups are active in the eastern Congo and are fighting for control of the country’s vast mineral resources, such as gold, the main tin ore cassiterite, and coltan (columbite-tantalite), which is used to make many electronic devices, including cell phones.

Since early May 2012, nearly three million people have fled their homes in the eastern Congo. About 2.5 million have resettled in Congo, but about 500,000 have crossed into neighboring Rwanda and Uganda.

Congo has faced numerous problems over the past few decades, such as grinding poverty, crumbling infrastructure, and a war in the east of the country that has dragged on since 1998 and left over 5.5 million people dead.

GJH/MHB

CHELSEA

Samuel Eto'o amwaga wino Chelsea

KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza,imethibitisha kumsajili mshambuliaji machachari raia wa nchini Cameroon, Samuel Eto’o aliekuwa akikipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala. 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 imefahamika kuwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo kwa dau la pauni milioni 7, japokuwa atapunguziwa mshahara wake kutoka ule wa awali alikuwa akiupata kwenye kbalu ya Anzhi Makhachkala,akiwa ni mchezaji pekee Duniani aliyekuwa akilipwa hela nyingi.ikiwa ni dau la pauni milioni 17 kwa mwaka.

 Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekata tamaa ya kumshawishi mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney baada ya ofa zake kutupiliwa mbali na Kocha wa Timu hiyo,David Moyes na sasa akaamua kumgeukia nyota wa Kiafrika,Samuel Eto'o.

Mourinho na Eto’o sasa wanakutana kwa mara nyingine,kwani walishawahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Inter Milan na kutwaa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.

REDD'S MISS ILALA ATOA MSAADA WA VITABU VYA SH. 300,000 SHULE YA MSINGI GULUKA KWALALA,UKONGA,DAR

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, August 28, 2013 | 12:45 PM


Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel amkimkabidhi  vitabu mwanafunzi Charles Costantino ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Shule ya Msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mollel alikabidhi vitabu 30 vyenye thamani ya sh. 300,000. Wanaoshuhudia ni Miss Ilala namba mbili Alice Issack (wa tatu kushoto), mshindi wa tatu Clara Bayo (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Mketo.


Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel akiwa na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada wa vitabu  30 vyenye thamani ya sh. 300,000 kwa Shule ya msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Warembo wakifurahi pamoja na wanafunzi.


Mshindi namba tatu Clara Bayo akizungumza na mmoja wa wanafunzi.


Mollel akimkabidhi zawadi shs. 5000 mwanafunzi aliyejibu swali walililoulizwa wanafunzi


wakiwa katika piacha ya pamoja na wanafunzi pamoja na Mwalimu Mkuu.


Warembo wakiwa na mwalimu wa shule hiyo, Lugano Mwaikambo ambaye aliwahi shiriki Miss Morogoro mwaka 2000.


Warembo wakicheza michezo mbalimbali na wanafunzi wa shule hiyo.


 



Warembo wakicheza Nage na wanafunzi

Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 waingia kambini - August 26,2013

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, August 26, 2013 | 10:14 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiI93GPnqjYsW4WmV6WSd0Ky9Cove5mZyO9o2mH4ftsZ6nqymBMtA4TwFOqmsyFm0x77sWYdCm52ZT5d6NREZ0O0A3Rrd1jHep7eTG77m3LZz_p5Dil5PQEOMzyZiWB5MushLHPUsA0YmWq/s1600/MMG20734.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akiwa pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Victoria Kimaro wakiwapokea Warembo wanaoshiriki shindano hilo wakati wakiwasili kwenye Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam - August 26,2013 tayari kwa kuanza rasmi Kambi yao.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvTFk2_8DeCQnzbUUPgvME8GwFBhM-_4wvZehsrT5-JKJ6Gvn-g3VXcMfjSAlKaHZNcfHpm76UMqP7DyI68l9acmeupNkbelS9lOBlcZ1WvgQ_3Blg7nz6yPnXgOLltV4RL-gPOxBAVgKm/s1600/MMG20757.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa kuwakaribisha Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 walioanza kambi yao rasmi - August 26,2013, kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhd3GC8ao-ZvkGHhEGj8nl3FX_wj9RP61pYK0tlLVG3jZOiyOqykAwRbREMDa6Hw82-lVFkJqKGoEZKH8ugPs3l_odHmJJXSXdzGZd7yIP3GU33vK4qgNJW11Q4cjQhATWYk0lJK5n65htz/s1600/MMG20784.jpg

Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Victoria Kimaro akizungumza machache wakati wa kuwakaribisha Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 walioanza kambi yao rasmi - August 26,2013, kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgiii9Ze1PlzPMPazDw_rvaaiA5-ZDVCKHT4KHbaJQvXCGRw0NuzF6LL5eUK_vqj2ANsA-ChGemOLRxNUh4LLVxoCiF2yosmf_IaL0Fm0U51ZPZzqpqmbvqEs8ja2z7eT8VtlUwJ1NkAmmi/s1600/MMG20822.jpg
Warembo wakiingia hotelini - August 26,2013.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhm2wdsY0gB5_sDj8OW6Pnqd9NFPy2HogS_Olb5XQRdPmR7pi3be3zO-ORLm9lY6NOzWwd_YZnTDwuuMHbwfoEFmoaAWOUqSLVpqgNNU3df7hLnKq7twJG9TSgTLmZbjTg2GgaYfw-0E3i3/s1600/MMG20831.jpg
Mkuu wa Itifaki kwa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa maelekezi kwa Warembo hao - August 26,2013.
 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger