Sema Naye: Label 6
Headlines News :

NEWS

Latest Post

Showing posts with label Label 6. Show all posts
Showing posts with label Label 6. Show all posts

Mwanademokrasia wa kweli hahitaji vurugu

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, October 11, 2013 | 9:52 AM

http://www.nationsonline.org/maps/political_world_map3000.jpg

KATIKA jamii yeyote iliyostaarabika, kutofautiana kimawazo ni jambo lililo la afya katika maendeleo yake ;na ndio msingi wa kupata wazo bora na linaloweza kuboreshwa katika ushindani wa hoja.

Ni tofauti hizo za mawazo kwa wastaarabu, hujenga maslahi na vikundi maslahi katika jamii na hata katika mifumo ya siasa na vyama vya siasa duniani kote.

Ndio maana katika nchi yenye demokrasia, ikiwemo Tanzania, uongozi hauna budi kusikiliza sauti na mawazo mbadala, ili kupata wazo bora linalokubalika la lenye maslahi kwa wote.

Kwa hili, hatuna budi kuipongeza Serikali na hasa Rais Jakaya Kikwete binafsi kwa kuwa kiongozi mwanademokrasia, aliye tayari kusikiliza mawazo ya pande zote, hata kwa wanaomzushia.

Mwishoni mwa wiki iliyopita katika hotuba ya kila mwisho wa mwezi, Rais Kikwete aliendelea kuonesha alivyo mwanademokrasia wa kweli, pale alipowaambia Kambi ya Upinzani, kuwa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Katiba, yanazungumzika.

Aliwaambia kwamba hata baadhi ya maoni hayo, yangeweza kukubalika kama wabunge wake wangekuwepo bungeni, ambako ndio chombo cha kuwasilisha mawazo mbadala na kujenga wazo bora.

Alisema bahati mbaya hawakuwepo, hivyo hapakuwepo mtu wa kusema mawazo yao na baada ya kupoteza fursa yao halali, kutaka kupata ufumbuzi nje ya Bunge ni jambo lisilowezekana. Alisisitiza kuwa masuala yanayohusu Bunge, hujadiliwa na kuamuliwa bungeni na si vinginevyo.

Pamoja na kambi hiyo iliyoundwa na NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema, kupoteza fursa halali ya kutoa maoni yao bungeni, ambayo hutumiwa na nchi zote zilizokomaa kidemokrasia, Rais Kikwete amewapa fursa nyingine ya kukutana nao kati ya Jumapili ya Oktoba 13 mwaka huu, ama Jumanne ya Oktoba 15.

Uungwana huu wa Rais Kikwete kwa kweli ni wa kuungwa mkono, lakini pia unapaswa kuigwa na wanasiasa na vyama vyote vya siasa, kama kweli vinataka kushika dola na kuongoza taifa ambalo msingi na uimara wake ni umoja, mshikamano na undugu unaostawi katika jamii yenye utii wa sheria.

Tunasema hivyo kwa kuwa kila mmoja ni shahidi kuwa vyama hivyo havijakomaa kisiasa, kiasi cha kupewa dola, ambayo kuiongoza lazima watu wake wawe na umoja, mshikamano na udugu utakaostawishwa na uongozi unaoamini katika utii wa sheria.

Hakuna ambaye hakusikia viongozi hao, ambao baadhi yao wamewahi kuomba kura ili waongoze taifa hili, wakitamka hadharani kuwa watahamasisha Watanzania wasitii sheria na kubatiza Oktoba 10 mwaka huu kuwa siku ya kutotii sheria.

Tumejiuliza hivi kweli kiongozi anayetaka kuongoza taifa hili, kama ameiva na kukomaa kisiasa, anaweza kutangaza siku ya kutotii sheria?

Siku ambayo haina tofauti na kuhamisha watu kuvunja na kuiba mali za walipa kodi wanaowapa viongozi hao ruzuku kila mwezi kupitia vyama vyao?

Tumesikitika kuona viongozi hao wa vyama vinavyoungwa mkono na wananchi, wakihamasisha wananchi hao hao wasitii sheria, lakini tumefarijika, kusikia wamekubali busara za Rais Kikwete za kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao.

Tunashauri kukitokea tofauti tena, ambazo tuna hakika zitatokea katika mambo mbalimbali tu kwa kuwa ndivyo jamii iliyostaarabika ilivyo, basi tuepuke kutoa kauli za namna hiyo, za kushawishi wananchi wasitii sheria, kwa kuwa ni kauli za jabu ambazo hakuna mwanademokrasia makini anayeweza kuziunga mkono.

MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUZINI MWA AFRIKA WAFANYIKA DAR

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, October 10, 2013 | 9:31 PM


 Katibu Mkuu wa sasa wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu Willson Mukama, walipokutana kwenye Mkutano wa sita wa Makatibu Wakuu wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Mohamed Seif Khatib
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahmani Kinana akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha FRELIMO cha Msumbiji, Philipe Paunde wakati wa mkutano huo
 
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Makatibu wenzake wa NEC, Zakia Meghji (Uchumi na Fedha) na Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni ) wakati wa mkutano huo. nyuma ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sixtus Mapunda.
 
 Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Dydmus Mutasa akiwa kwenye mkutano huo.
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama akisalimiana na Dk. Asha-Rose Migiro wakati wa mkutano huo.
 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya Watu wa China, Ai Ping, wakati wa mkutano huo
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Ai Ping wa chama cha CPC cha china wakati wa mkutano huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar), Vuai Ali Vuai
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaelekeza jambo, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati wa mkutano huo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuanza kwa kikao hicho
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, leo kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 
Mkutano huo ukiendelea katika hoteli ya Kunduchi Beach

Mwenyekiti wa Mkutano wa Sita wa Vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha mkutano huo, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
 
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mkutano huo
 
 VIONGOZI wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, walioshiriki kwenye mkutano wa sita wa vyama hivyo, leo kwenye hoteli ua Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam, Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Didy Mutasa, Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chana Cha Kikomunisti cha China, Ai Ping,Katibu Mkuu wa MPLA cha Angola, Julio Paulo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama cha FRELIMO cha Msumbiji, Philipe Paunde na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia,Nangolo Mbumba
 
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waandamizi, baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF, Didy Mutasa akionyesha alama ya hamasa ya chama chake, alipozungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi mwa kusini mwa Afrika, kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana na Wanne kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, September 25, 2013 | 7:09 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIaGrYfY3q77_fkd80Fk0PbcU3ypkh-d-dTpDx7bXaongpN2lVpvCBS9Oi_jOlD7z9_Wu_T7a5Z1ZoFdERf1BZSCUdOcHPib1fCIxRzrBVKEyzNTxLozSUwLrPnHmLDd_3UpQS2gBTCbDI/s1600/1.jpg
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPSb9XD6BJdAnJq5A2BchcIb5uoG-bkavVad_a12jk052-HVQSqLsnUw3OvWbAZZmFk91LZO7LyU7jFvmL8SStVAwnK3TMbmXSg5vvhwQmD7A76sGi6TlxTgKWfGrOoeDDytIrKi3jLgUV/s1600/5.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8o2XoL6AOr5p9n7xyg1NlWM-4Yy3n5aV-bQSb7OZwupw9wu1gCRe9LhW6zFXCbz6lFVLAUsvVIo58uTVjw4VSadBamHrjOr1cLud08Q-GtRKDChx92r6SwsQuPTNBTPnDRoI_qvIgGJX2/s1600/19.jpg
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhElsLK74QqLSQfC4nPcyTboPgy_DM5IM4m5vyxguI9xwuXxD2S8CepMRZzZqM83fWyRLZ3GM4e21eQ7aUDU5eRay8KWDCKMwCJcNncFNVQsU8bBNS6334TXPEy8omCcw2BlIG4orocEV9X/s1600/16.jpg
Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfqmojlgFLNAH4qBJ4gjh0XUBp7PdNBLFxVM5xIGFd2_XjlYSP76T-CPKQwJ5LBc4crOlu5g2kXbowKzV9tN_MWrLznEnt-KJ2Ty5SkDnj8kOyfql3A-X3RnM9UJUWOfP5aICie4D49oLm/s1600/12.jpg
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgRGLNTqduM3sPJFV06zdHOYceT9Hc4hSHJKLzB_YCwOIHO-pKxZrcBplKAPRmkIafXX_g0qTDYKPNzu0bal9QR2_KwE-QQpY5BC1rD3q-Y6GCqe_EM0ZyYGUMASN_SWNB8kep7kvmjleV_/s1600/13.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkLI8Ot4VoH5VKaVfhC1Uvj83XX2aKLNz3c4eKPugPw1i9kYsrzHx5K8AkoavsZbnDNwf9-e9c4xeW1UVltw5aYG092n3M8IOsKNjN5FR0XmTEiJ_R3r5W5T5DJIrFHG-nNU5s5tsGzqgg/s1600/7.jpg
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiH6vLtV5XrBon5YeAbgtl4jSQHnt3cYiDUTLWJ0G7LNJX6zJoCetGT6keqZUFkFpkmx-JLUZHiw_Vt-3db5-91AhLQzOJ1Q2peSPI_3vGmpTt9Fg28MlsdJWv1f8u8tgiALv5hckQfhEs8/s1600/8.jpg
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwArlombfD7pNj_mA5SF1vOdvVyBg_WTmSuu9RxfrqucnFo7hd4xxhZsOimUi5jzpF161jSeLgJsc-YNU81rMQcpYgj-Xfr5erEpsStZS1oGT22RnKb3EOD35VwLo-DpRQB3br8FVJW_33/s1600/10.jpg
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8u2wyoWH_5xo1Ux1pZI0_HFlfwK5I3aOouakoLNxKzAdoZGi73l91zHk8iD9JCAxcJ142iyUdK_cjvuC5z9P7HbDPfdoj2N0XdvWkpuh6znHBGOyj4x0OkM0O7Mthu_wfvGPu7Olss86H/s1600/18.jpg
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.

CCM YAPOKELEWA KWA SHANGWE NA NDEREMO SHIRATU

KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiJo3zM2_opOo5IvKxpgCtFvBLeaOX9CPZWRq6yEeUmbRBzsnD-1FFmoKOGibgU50HFxwgmLSlPH5tufmJ488Gdt_Wdx7EpKdFePnQf46fD3zRSnvdQKNjsjpLMSc4NuN58BkQEWT3EXbB/s1600/gz1b.jpg
Mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSlcZDP1GEEbM3lgX55ZaVQ8Rl4gEKIfHev9Th8X4CiC3W8TnLe8G06cQB-TC7VaNsiBWH3cgaS2QuBqZmWDLSDh19d_lsFyhNtEOPukrVXEXf6rG8vCWB_vN4bBRVQIBHfUdBfMDnjEEJ/s1600/gz3b.jpg

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na mshikamano walio nao.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSMXH7HPbLb4TDVvZpwI_3ntXJ5JARChn02WOPbIlO3a76KQ8hxzymjfdKTNKNXQ_UIY5_4KjjeyZlci0MGvxi4ufKpaMeHdTNNiQNHcTbK5I6ocVeWHBQV3BZ3UZojuXXT34LCbm-PBE0/s1600/gz4b.jpg

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgEWvHGV95cNDnwHBkEQNwgSrDkFQcuAuH_DYC41-54KF_gvX9ZRWk3d6VnNVohesdWj-vh6LFGWxnPqYh3Tq1l-WgIZcACnRPeNSFNgIAcMZgObFbrp_tGmLv1Wfs5bHZb8G8lxUxmrQAS/s1600/8.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote za kisheria.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDxzQjXdm0ZPLNSlOJAZHNExBg2F37Pn74ew1klHLlQeJZqHlpESTJgrHCqCjRZL91RQEeQTtjRrW90BWtipEt58dB7c95V2nOZ6GmkldZSvuQPzYfBqZoxLxHYiKGYLCrAmWxyMXPBgor/s1600/1.jpg

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVlfSejiHq1Vqwp5nriIomBn9sRpX43iZpHHVo0-yT5KE3A_la564fXM3YuG267U-MfL0hGCZKrotsc-eT-qq_uWiKfvVdK13o7PBhXI5TTXss7WARhvdJGJrH549ikkk0VfVu0WslD1mt/s1600/gzb11.jpg

Sehemu ya Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba 2013.

HAKUNA KAMA CCM NYAMONGO TARIME

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 23, 2013 | 2:27 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtZLpYPERIZzMV-nW-OD1YPue5DOel0jscq8fXJGGafRWKV6sCK1WWhBhgPRcFgZGySlBHtTAkFh16jFLwaB5QtR0CgZf-Tn0Dj8kMQo7mZq95r2cOc3HaW_4RZF-ai7A4KQgicstVkD1u/s1600/1.jpg
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-eQAAU-l8g-hKHsbGkv0lqaMHmc2BbB_GePKNs39vki5LVB51N2japYcEwF0JrUUEDRKCfnw6UqLvqivsZkCuhK79Yhm8yrWvNVjkKFNKSqi-wimfEXmrvt4OaYyqi2fx303vEl6yrn0f/s1600/9.jpgOfisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_yMQUyEoE5l2jEvWlp1qhCteLrEtiec5OSrPU_YRHr6ouM-XMlVgc1vHYst_Zb6zv0p2T4nmjmCNiEjikPVNZRIjGbeItIoEAAyleQIcP_mnQv3DbSGoP8bxBMGOPyKUJyrZnIiIPD7GG/s1600/2.jpg Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara .

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNZI811vjvnLleIvXRT6OX4QipDnxNa48NsR-AyhwnT6OxeyIhM7uP9ogc0z1lmHLxeMoir4-R5SwgX5ezct_qjcjWHBzv5FAYFCx48fSQiqOf48Eeeae_Odsxc8XRY64N0yE5oZX8Brro/s1600/3.jpg Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFE2jB7TdGuzssKNmNPUrEZYvp-QlnfTjGBwvzqkMwephZlhESrQ8RhQ4DkaCP8OnzXXLGoAQ9MoGdszXIno4ID2OF0KmSHRGzNasiU1k6ujKY-38tKShtJxY2ws1GvQerLJRYcBU5Z3Pu/s1600/5.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-D5FCYLzYld1G4Dj_iB_BWYmy6DoV812Z8DM-NyXy9z9jlsZretDXN9d5UTyx8koFE6eWoUNopwucArNFAH23yKU2s8RpP_W_DYtIrIUBzxo5x1Xi1Mu-yOqWmKdRQc-Exr5bgnBCLwR_/s1600/6.jpg Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGqs0pSYgFcCZwzcTPO6oEMoZdDrUW39KCZc4-6tT-VF9YDH-fuqeXYnU9I5mwoHlNyzHvtaU-zxuySUObWu_tREqOC3Ni5q7s98xCDGqyG-1dfq5l377QO3JcsdNI82U-X8SRUnoeYucC/s1600/7.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBqIBKR_Rdq1juA7xhMevzQlbGLpi6J26iB_SsucINTR5yNagSW8YWyiJWHEMuF303obJvtY_ImvV8dC5mIJGPN8G25AnthY1RmDrP-xepBiC0I90h25bXZKCmg1Fnf1crhxSyroiN4W3t/s1600/8.jpgKatibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnP-NXduic4PmvHTGMOuH4JBvwfOgoA3qA0HQ3yYe0c7vy-Ucq6ebkKqFQd03dFDL99Fqd0vcyICwGNI_dCgaSRLMcz_COdOcQ3_Xc1c2S5a_29tsEeHj5cMbGkfDhoqiUSr2VN-mm8_xS/s1600/10.jpgSehemu ya wakazi wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya kuyatatua.

==== ======  =====

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,leo amefanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara .


 Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.


Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.


Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi.

KINANA ASHUHUDIA MAABARA INAYOTEMBEA WILAYA YA SERENGETI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYXduRpBJkBWNjP9duCNQ-rBUNYl_Wc7K6v45dBpQ3EqQEWztrSZdO5_csUT2A45yAnhPUQKtQ48gxSfueXcsYPNkW2EPFXHiqfmSR8rt-vRXFfunmRqK2zvZ2l_1v0ITpKJ6LADBp87W4/s1600/10.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa kata ya Isenya wilaya ya Serengeti waliokuja kumpokea.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgq17nnM9iU0FeVNVralCrD3Q4aVn5o5uHhBlhQBFd1gaYizy2AvWJSS8wL6CRifC6RZGaqKOVACxE2u364jHPoWndbJSkLUYQAXXJUVBSx_p9CCXnhrlI3l90RI8WLfco4eZr5B6bd0Gm4/s1600/11.jpg Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwalimu wa masomo ya sayansi Ndugu Silvester Joseph , Katibu Mkuu alitembelea shule ya Natta Secondary na kushuhudia jinsi masomo ya sayansi yanavyopewa kipaumbele.
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Peter Semion wa shule ya sekondari ya Natta iliyopo kata ya Natta wilaya ya Serengeti akimuelekeza namna ya kutengeneza sabuni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shule hiyo ya Natta iliyopo wilaya ya Serengeti.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoOkTaiUOVumEm2FPb7XATNVSqKcMiOL1vVbSxFNGVMyplF43cjGiktWQ8w3TkNWqmSu1c4LJOBn-qwHQ7waXJR1XM0Cj79NuwvkkwCRlugfMzaXB50dsOk8qX70XupKK00q8cl4OcGpIw/s1600/8.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wajasiriliamali wa kuendesha boda boda na ukulima wa mboga mboga mara baada ya kuzindua kikundi hicho ambapo aliwasihi lazima wapate elimu ya biashara wajue namna ya kuweka na kukopa na kulipa madeni kwa wakati.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi14HD6f76zvfBNfCfO9OTJ0U0PXCYKKKvfNAF0shdq7elU5sSdkn3nxDCRPddaJ_t24GaiNIukkSe1k9dRzxJRTvEgGTa95EUzsLUGRxNmA1JgMQpChroMxiPUXAaNlug0P5j0vi5iTlUB/s1600/9.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya ukumbi wa mkutano wa MUGUMU CCM ambapo alikutana na vijana wajasiriamali wa wilaya hiyo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhO6SZ3GIC5Zhk7MJDPWuRbgMdcjZwvhv-9qFU3aL8be_TcqmLV-pa259S6b6CbwtaPh8ydXq-NXyvF3wEH3aYJSer5w7LEmuCo1qySfkd4GrmtnEtIMhfdPKg_Mx82tzdDIOpJom-DIBQx/s1600/4.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Natta mara baada ya kumaliza kikao na balozi wa shina namba 11 Tawi la Natta Majengo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEif2t_Eec9vjUrxShyzIyXHs06KQC9bbO7oui8wkfFbubsQQLypn2eEklbtYbmp3EIp2WFow_xQyUBWn9L9yg2hIX1unsraF_7TrDgT6ui3kyDJmBD-y1f53EsLNNSST8mu3PZHZVLA7Bcp/s1600/5.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani kwa wazee wa Natta baada ya kumpa heshima ya kuwa Mzee wa Natta.
 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger