MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUZINI MWA AFRIKA WAFANYIKA DAR - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUZINI MWA AFRIKA WAFANYIKA DAR

MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUZINI MWA AFRIKA WAFANYIKA DAR

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, October 10, 2013 | 9:31 PM


 Katibu Mkuu wa sasa wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu Willson Mukama, walipokutana kwenye Mkutano wa sita wa Makatibu Wakuu wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Mohamed Seif Khatib
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahmani Kinana akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha FRELIMO cha Msumbiji, Philipe Paunde wakati wa mkutano huo
 
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Makatibu wenzake wa NEC, Zakia Meghji (Uchumi na Fedha) na Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni ) wakati wa mkutano huo. nyuma ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sixtus Mapunda.
 
 Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Dydmus Mutasa akiwa kwenye mkutano huo.
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama akisalimiana na Dk. Asha-Rose Migiro wakati wa mkutano huo.
 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya Watu wa China, Ai Ping, wakati wa mkutano huo
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Ai Ping wa chama cha CPC cha china wakati wa mkutano huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar), Vuai Ali Vuai
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaelekeza jambo, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati wa mkutano huo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuanza kwa kikao hicho
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, leo kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 
Mkutano huo ukiendelea katika hoteli ya Kunduchi Beach

Mwenyekiti wa Mkutano wa Sita wa Vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha mkutano huo, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
 
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mkutano huo
 
 VIONGOZI wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, walioshiriki kwenye mkutano wa sita wa vyama hivyo, leo kwenye hoteli ua Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam, Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Didy Mutasa, Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chana Cha Kikomunisti cha China, Ai Ping,Katibu Mkuu wa MPLA cha Angola, Julio Paulo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama cha FRELIMO cha Msumbiji, Philipe Paunde na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia,Nangolo Mbumba
 
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waandamizi, baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF, Didy Mutasa akionyesha alama ya hamasa ya chama chake, alipozungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi mwa kusini mwa Afrika, kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana na Wanne kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger