RAIS KIKWETE AZURU WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA - SEPTEMBER 10, 2013 - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » RAIS KIKWETE AZURU WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA - SEPTEMBER 10, 2013

RAIS KIKWETE AZURU WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA - SEPTEMBER 10, 2013

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, September 10, 2013 | 7:38 PM


Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati akisomewa taarifa ya Wilaya ya Kwimba na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Seleman Mzee huko Ngudu makao Makuu ya Wilaya  -Septemba 09,2013.



Rais Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na hoihoi wakati alipowasili kwenye Chuo cha Michezo Malya kilichoko wilayani Kwimba  -Septemba 09,2013.

Rais Jakaya Kikwete akipokea taarifa ya ujenzi wa uwanja wa ndani wa michezo wa chuo cha michezo cha Malya kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Ndugu Allen Allex. Rais Kikwete baadaye aliufungua rami uwanja huo.

Rais Jakaya Kikwete akizindua rasmi uwanja wa ndani wa michezo kwa kukata utepe. Walioshika utepe huo kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Malya Ndugu Allen Alex, Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamadunu na Michezo, Ndugu Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve na wa mwisho ni Mbunge wa Kwimba. 

Mkuu wa Chuo cha Michezo cha Malya Ndugu Allen Alex akimwelezea rais Jakaya Kikwete ramani ya eneo lote la chuo mara tu baada ya uzinduzi wa uwanja wa ndani wa michezo.

Rais Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na hoihoi wakati alipowasili kwenye Chuo cha Michezo Malya kilichoko wilayani Kwimba -Septemba 09,2013.



Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wa Kisukuma zilizokuwa zikicheza wakati Rais Jakaya Kikwete alipofika tu uwanjani hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara huko Ngudu  -Septemba 09,2013.

Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kituo cha polisi cha wilaya ya Kwimba mjini Ngudu  -Septemba 09,2013.



Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Ngudu muda mfupi kabla ya kuwahutubia.

Rais Jakaya Kikwete akiangalia na kupata maelezo ya mchoro wa mtandao wa maji katika mkoa wa Mwanza yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wa hadhara mjini Ngudu.





Rais Jakaya Kikwete akitawazwa na kusimikwa rasmi kuwa Kamanda Mkuu wa sungusungu nchini na Chifu Shimbi Martin Morgan wa wilaya ya Kwimba.Katika sherehe hiyo Rais Kikwete alikabidhiwa kofia nyekundu, mgolole, upinde na mshale pamoja na silaha nyingine za kijadi.

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti na fedha taslim shilingi laki tano Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Kwimba ndugu Rhoda Joseph Michael kutoka kwa mkuu wa wilaya baada ya muuguzi huyo pamoja na daktari Makori Josephat Maro kuamua kutoa damu yao kwa ajili ya mama aliyekuwa mjamzito na kuwa na upungufu wa damu wakati wa kujifungua baada ya ndugu wa mama huyo kushindwa kupata damu inayofanana naye. Rais Kikwete aliwazawadia sh milioni moja na nusu kila moja kwa kitendo hicho. Picha ya pili Rais Kikwete akimpongeza daktari huyo.

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Kwimba huko mjini Ngudu ili kuhitimisha ziara ya ya siku moja wilayani humo  -Septemba 09,2013..PICHA NA JOHN LUKUWI
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger