Rais Kikwete atembelea mji wa Vallejo, California
Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, September 19, 2013 | 7:06 AM
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Vallejo jimbo la California nchini Marekani leo wakati Rais alipotembelea mji huo wa kibiashara kwa mwaliko wa meya wa mji huo Mstahiki Osby Davis.
Meya wa Mji wa Vallejo lililopo katika jimbo la California nchini Marekani Mstahiki Osby Davis akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa mji huo leo tayari kwa sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa ishirini ya ushirikiano kati ya mji huo na mji wa Bagamoyo.
Mjumbe wa Kamati ya ushirikiano kati ya mji wa Vallejo na mji wa Bagamoyo Bi Dinah Villanueva akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete hati ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya mji wa Vallejo na Bagamoyo miaka ishirini iliyopita.Ushirikiano huo uliasisiwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Madini na mbunge pamoja na kamati ya wajumbe kutoka mji wa Vallejo California. Katikati akishuhudia ni Meya wa mji wa Vallejo Mstahiki Osby Davis.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago cha umoja meya wa mji wa Vallejo Mtahiki Osby Davis wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya miaka ishirini ya ushirikiano kati ya mji huo na mji wa Bagamoyo (picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment