KINANA KUKOMESHA UMANGI MEZA WA WATUMISHI WA CHAMA NA SERIKALI - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » KINANA KUKOMESHA UMANGI MEZA WA WATUMISHI WA CHAMA NA SERIKALI

KINANA KUKOMESHA UMANGI MEZA WA WATUMISHI WA CHAMA NA SERIKALI

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, September 21, 2013 | 3:00 PM


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa gwaride nadhifu la chipukizi wa mkoani Mara.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Ndgugu Stephen Wassira mara baada ya kukagua mradi wa kusambaza maji kwa wilaya ya Bunda


Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na wananchi wa kata ya Kibara katika jimbo la Mwibara alipotembelea kuona jinsi ilani ya uchaguzi inatekelezwa.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kufungua kwa mradi wa kujenga chuo cha ufundi fundi Stadi katika jimbo la Mwibara,kulia ni mbunge ndugu Kange Ligora na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa ndugu Christopher Sanya.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimimina zege kwenye shughuli za ujenzi wa chuo cha Veta cha Namibu ambacho ni sehemu ya kazi nzuri ya mbunge wa Mwibara Ndugu Kange Lugora.


Mbunge wa Ludewa akisalimiana na wananchi wa kata ya Kibara ambapo alitoa pongezi kwa ujenzi wa chuo cha ufundi na kuongeza nguvu akachangia mabati mia tano pamja na siment  mifuko mia moja.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchi Ndugu Amina Makilagi akisalimia wakazi wa kata ya Kibara , akingea ujumbe mmoja tu alisema wakazi wa Bunda acheni kuua wakina mama wazee kwa tuhuma za uchawi alichukua nafasi hiyo kukaa kama wanandugu na kukomesha kabisa mauaji hayo .

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa jimbo la Mwibara na kuwaambia maendeleo hayaji kama mvua kwa siku moja ni muhimu kushikamana na kushirikiana na viongozi wao katika kutatua na kuleta maendeleo yao.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza maandamano ya kuelekea kwenye viwanja vya mkutano baada ya kufungua shina la wajasriamali wakereketwa wa Pamba road.


Mbunge wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  ( Mahusiano na Uratibu) akihutubia wakazi wa Bunda kwenye mkutano mkubwa wa CCM uliokuwa unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM


Mbunge wa Ludewa Ndugu Deo Filikunjombe akiwasalimu wananchi wa Bunda wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu alihudhuria.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Bunda waliofika kusikiliza mkutano huo.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu uliojazana kumsikiliza katika viwanja vya Bunda.


Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa zawadi za kumtambulisha kama Mzee wa wilaya ya Bunda.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa mkono wa shukrani baada ya kukabidhiwa zawadi za heshima kama Kijana wa Wilaya ya Bunda.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana anaendelea na ziara yake na sasa ameingia katika Mkoa wa Mara na tayari ametembelea shughuli za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya ya Bunda.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alianza kwa kupokea taarifa ya hali ya kisiasa wilayani hapo na kisha kutembelea mradi wa maji ambao umekuwa ukilalamikiwa muda mrefu kuwa unachukua muda kukamilika,katika mradi huo amekuta hatua ya kwanza kuwekwa kwa bomba kubwa umeanza ,pia alipata nafasi ya kutembelea jimbo la Mwibara ambapo alishiriki katika ujenzi  wa madarasa ya chuo cha ufundi stadi Namibu na kutembelea shule ya Sekondari Mwibara katika kata ya Kibara pamoja na kutembelea kiwanda cha Mara Coooperative 1984.

Ziara hiyo wilayani Bunda ilihitimishwa kwa mkutano wa hadhara ambao ulijaza umati si wa kawaida.

Katika Mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema  tangia Kinana amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mabalozi karibia nusu wamekuwa wakifika ofisini kumpa pongezi bila kificho na kuonyesha kufurahishwa kwao kwa uteuzi huo “Nawashangaa watani zetu kukomalia suala la balozi wa China wakati huu wakati ambao tumefanikiwa kupata ufumbuzi  wa matatizo ya wakulima wa Pamba”,aliendelea kusema mabalozi wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za CCM ikiwemo kuwa wageni waalikwa kwenye mikutano mikuu ya CCM na hiyo yote haijawahi leta maneno, Akasema msajiri wa vyama ameshauriwa vibaya kuhusu hili.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ameendelea kusisitiza juu ya madai ya walimu nchi nzima kulipwa kwa wakati bila kuwa ya malimbikizo,alisema tatizo hili la muda mrefu na Rais alishatolea maagizo  lakini halitekelezwi akasema kama Katibu Mkuu wa Chama anatoa miezi sita walimu wawe wamelipwa madai yao na kama halitofanyika yeye kama Katibu Mkuu atalipeleka kwa wabunge wa CCM kasha wapitishe azimio Bungeni la kufukuzwa kazi wahusika.

Katibu Mkuu alisema “ watu wamekaa mjini wanalipwa vizuri, magari mazuri na suti wamevaa lakini hawajali wenzao wanajilipa posho kila kikao”

Katibu Mkuu alisisitiza kuwa anamuomba Waziri Mkuu azuie vikao wakati wa kazi na vikao vyote vifanyika baada ya muda wa kawaida wa kazi kumalizika.

Alisisitiza yeye ni Katibu Mkuu wa CCM anayefanya kazi kwa vitendo na amedhamiria kuhakikisha chama kinafanya kazi nzuri ya kuiongoza serikali

Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger