KINANA AMALIZA ZIARA YAKE BARIADI
Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, September 19, 2013 | 12:11 PM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa Doto Nchege mwenyekiti wa kikundi cha waendesha bodaboda wa mjini Bariadi baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba mjini Bariadi
Waendesha bodaboda wakiondoka na pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya sabasaba mjini Bariadi katika ziara yake ya mwisho kwenye wilaya hiyo mkoani Mkoani Simiyu ambapo kesho atamalizia katika jimbo la Busega na kwenda moja kwa moja mkoani Mara tayari kwa kuanza ziara nyingine ya siku sita mkoani humo.
Nape nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na uenezi akiwahutubia wananchi wa Bariadi katika mkutano huo uliofanyika mjini Bariadi leo.
Nape nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na uenezi wa pili kutoka kulia akifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Sabasaba mjini Bariadi leo, kulia ni Dk Titus Kamani Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu na kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima na Pasacl Mabiti Mkuu wa mkoa wa Simiyu.
0 comments:
Post a Comment