Sema Naye: Label 7
Headlines News :

NEWS

Latest Post

Showing posts with label Label 7. Show all posts
Showing posts with label Label 7. Show all posts

JK azindua Shule ya Sekondari ya Miono, Bagamoyo

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, October 10, 2013 | 2:09 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_awpBaYQqirujVbU7QiaLJkT9DExXJpZZO5fYVvc7ZF6eFT5tdrxJmieYTmdrlh4xoPtnJA0n67Fib9HqBkMib79Ya0OcJVh2ecg7b6or6aN1_JZ194LpfAxa9FdZNoCq3y-PhLFLch5u/s1600/D92A6377.jpg
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuizindua rasmi shule ya sekondari ya Miono iliyopo Wilayani Bagamoyo, akishuhudiwa na  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe Philipo MulugoRais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Pwani.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPZxqMdiGvXFwzStao4h2kpaW5vwhIrQUnMtAQ9qDPxlidFVsbHTnyy5QmRZHpFFos0u59z-WMQViLSjst9TXPNCvweJ3VezmDEl5au1wBEzAwSbv-3yj9sVUsGrtcDaj2zyv2uj4LlhMK/s1600/D92A6347.jpg
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maktaba ya Shule ya Sekondari ya Miono Muda mfupi baada ya kuizindua shule hiyo jana Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEic3U7B_2IONJT23UHdZaOY7oWkDxa10uGhdTWDQgSNvBAfutjrSZrbrx3jzZpfUKfdVtIKu9LjCXtX9Y7ITZxTUq7FeIkBPDsh0z0QQq51l3_spF_W8byIAAaBZKCRjnix7VwMLcPqQlxj/s1600/D92A6311.jpg
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  wanafunzi wa kidato cha tano wanaosoma Shule ya Sekondari ya Miono Wilayani Bagamoyo, Nyekwabi Jackline George,Penina Odara na Magret Machinyita wakitoa maelezo ya jaribio la sayani somo la biolojia wakati Rais alipofungua rasmi shule hiyo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MONMOUTH HUKO NEW JERSEY-MAREKANI

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, September 25, 2013 | 6:19 PM


 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya kuwasili chuoni hapo. Kulia kwa Mama ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi akifuatiwa na Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ramadhani Mwinyi, na Ms Janet Mahoney,wa Chuo Kikuu cha Monmouth na kushoto kwa Mama Salma ni Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu hicho, Bwana Saliba Sarsar, Makamu Rais wa Chuo cha Monmouth anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na Mwisho ni Bwana John McLaughlin, kutoka Shirika la Footprints for Education International la nchini Marekani.

 Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth Dr. Paul Brown,akimtembeza Mama Salma Kikwete maeneo mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. 
 
Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. 
 
Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. 

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu  4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin.
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anazungumza na Bwana Kevin Williams, Mwalimu kutoka shule ya Asbury Park. Shule hiyo ina uhusiano na shule ya sekondari ya WAMA, iliyoko huko Nakayama, wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Katikati ni katibu wa WAMA Bw. Daudi Nasibu.
Picha zote na John Lukuwi


Na Anna Nkinda

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba chuo kikuu cha Monmouth cha mjini New Jersey nchini Marekani kufundisha wanafunzi wake lugha ya Kiswahili kama lugha ya kigeni ili wakazi wa eneo hilo waweze kuitumia katika mawasiliano pale itakapohitajika.

 Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ametoa ombi hilo leo wakati akiongea na uongozi wa chuo hicho alipowatembelea yeye na ujumbe wake.

 Alisema hivi sasa lugha ya kiswahili inakuwa kwa kasi na kutumika katika maeneo mengi hasa nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi nao wawafundishe wanafunzi wao ili wakienda katika nchi hizo iwe ni rahisi kwao kuwasiliana.

 “Kiswahili ni lugha ya taifa letu la Tanzania ambayo tunaitumia katika mawasiliano, mkiwafundisha wanafunzi wenu lugha hii nao watawafundisha wenzao hivyo itakuwa ni rahisi kwao kuwasiliana hasa wakisafiri na kukutana na watu wanaotumia lugha hii”, alisema Mama Kikwete.

 Kwa upande wake makamu rais wa chuo hicho Dk. Edward Christensen alimshukuru mama Kikwete kwa kutembelea chuo hicho na kusema kuwa ombi lake la chuo hicho kufundisha lugha ya Kiswahili wamelisikia na wataangalia jinsi gani watalifanyia kazi.

 Aidha Dk. Christensen aliwaomba wakufunzi na watu wenye utaalamu wa mambo mbalimbali kutoka nchini Tanzania kwenda katika chuo hicho kufanya midahalo na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho.

 Chuo hicho kinawanafunzi wapatao 6300 kutoka ndani na n je ya nchi 29 na kinatoa kozi mbalimbali zikiwemo za Sayansi na sanaa katika ngazi ya cheti, shahada na shahada ya uzamili.





Rais Kikwete azindua Mpango wa Kuzishirikisha Sekta mbalimbali kupambana na Malaria



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuAV6dDhIgTw_dUxlx5JEReti4GkuiXwTyxfd0uwJI8Wry6j0wI7PSvRueZBknrXnU3d7-zWWzeaNQx2Mjki8mIFootAEJ7c5cWfoJJCqYk8xKX__X2D2gSGh9mkzGPIHFKPK4pRn5oRcs/s1600/0L7C0016.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8QYccPbq2sfrf-Qm9CddccpJ2-TDwkLsgk7mPIexpOSsP7JiI5WecF6RczULIntksLBxDImRdIrJQqsWtaUc4tzAdSnGDG8TvFqsK4bd-wHHcYrpXSn0S6L_4o50hcId38ji0gmiyFf5A/s1600/0L7C0043.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kuzindua rasmi Mpango mpya wa Kimataifa utakaohusisha Sekta mbalimbali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria duniani. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani chini ya uratibu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Taasisi ya Roll Back malaria Partbership.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Waziri wa Afya na Ustawai wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi (Mb.) (kulia) wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Guebuza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuzishirikisha Sekta mbalimbali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
   Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Guebuza wakiwa na wageni waalikwa wengine.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula akiwa na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukabiliana na malaria kwa kuzishirikisha sekta mbalimbali.

Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Milenia, Prof. Jeffrey Sachs akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWJnm9x2R7sq2rAifQwtHzpm7j0GTnWUcQHenBJxL8i35UB1DXiUmpiSWRzMOc9KJ7LQOXueglxw3Ij0vtDS0lJjm3jzM5vwC72ZMQpw42qKKNiSrEYOJRAmA8LYyIYf6vY1qdVOSwG2BT/s1600/0L7C0046.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5S4zX9-5p0AH-5Gf23p0aMBaHqHwaQ0s0ncvP51fngi0MXQt6L-MRkID2Mluf4s_E9cpwtCaTxxI0MZxgSD1wda6BqsjsL_Sp_0I2G9GbBs8edhQovuJqiNnJ-q6gfrCp8Pu2cQwSbkiF/s1600/0L7C0045.jpg
Mwakilishi wa Taasisi ya Roll Back Malaria Partnership mjini New York Bw. Herve Verhoosel akimkabidhi Mhe. Rais Kikwete mfano wa kifaa cha kufukuzia mbu  wakati wa uzinduzi wa mpango wa mapambano dhidi ya malaria.

Mhe. Mwinyi akifurahia jambo na Bi. Rebeca Grynspan kutoka UNDP pamoja na Bi. Ellen Maduhu, Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania, New York.
Picha na Rosemary Malale

JK na Mama Salma wakutana na Michelle na Barack Obama na Melinda Gates


Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mwenyeji wao Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya viongozi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa 68 wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Picha kwa Hisani ya Rae Lynn Wargo wa  Umoja wa Mataifa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgk1Og_XYY0CvNWa_q-3X4wReUsxSdp_YG5QyTe3kS8TKF_NYNtw2HrtuUHEaYnrRIuCa8aEMoDpbfrkKP4sjT8cNJ1ng3zuYKRcqizUiLodVr2n54JigqoTuA88tozebV66hjhcNsn9I0W/s1600/0L7C0100.jpg
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama Melinda Gates wa Bill and Melinda Gates Foundation walipokutana katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York leo. Picha na Freddy Maro

PRESIDENT KIKWETE ATTENDS HIGH-LEVEL meeting on Scaling up Nutrition in New York

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, September 24, 2013 | 2:36 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmSL2mDBl72wx_UJPc4oCUMCO58qLKSbdb4rvKQPQ4Ir5vK9Z-XWzd-zk2mEXBHSbGaDG1YbZc9PvHNbHCqB_kULvwzeT6lKffc7FGvWx3GhOj13QZX_IpuXraRUh2-NXMJ2wh1wzdZ8XL/s1600/0L7C0168.jpg
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a High-level meeting on Scaling up Nutrition  in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhIBpBhOMZF7m0bPlOJpBCPVduh4FDmsNbJOweZJMl1bPMPGSTtND_JEcP8KFrcWjMp3GduPyIWxW7P58gqxYsdkMY9FD6HzYnH2N-F3uwVUG4DMCUpuNv18AF4y6L_6PgcgMEyLWDHaqc/s1600/0L7C0195.jpg
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a meeting on Scaling up Nutrition held in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member, behing hi with red tie is Tanzania's Minister for Health Dr Hussein Mwinyi, left is personal assistant to the President on Nutrition  Dr Wilbrad Lorri

Each year since 2010 there has been a High-Level Meeting and a series of other gatherings held in New York during the United Nations General Assembly, to increase political attention to the issue of nutrition and encourage greater support for the efforts of SUN countries and the Movement.

As a result of the dramatic increase in political attention to nutrition throughout 2013, SUN countries and stakeholder groups have sought to create space for more in-depth, structured interaction. The SUN Movement Global Gathering offers an opportunity for this form of interaction. Representatives from SUN countries and across the Movement will participate in the workshop-style event to solve practical bottlenecks and achieve concrete results.

The purpose of the 2013 SUN Movement Global Gathering is to enhance the Movement’s impact through:

*Demonstrating results in SUN countries – contributing to the learning agenda by focusing on how results can best be achieved;

*Enabling countries to seek solutions to help them scale up nutrition from other countries and networks;

*Bolstering mutual accountability within the Movement – with all constituents – countries, networks, Secretariat and members of the Lead Group giving accounts of their contributions; and

*Envisioning the Movement beyond 2015.

MZEE MWINYI AWAONYA WANAOTUMIA ELIMU NA UJUZI WAO KUANGAMIZA USTAWI WA JAMII

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 23, 2013 | 9:49 PM

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC_1114.jpg
Elizabeth Mwase Programu Manager wa Mtandao wa Watoto na Vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) akimpokea Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya pili ambaye alikuwa mgeni rasmi ya Siku ya Kimataifa ya Amani iliyoadhimishwa mwishoni mwa Juma jijini Dar es Salaam ukumbi wa Don Bosco.
 
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa jumuiya za maendeleo za nchi wa hisani wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC_1120.jpgMgeni Rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipokea mfano wa ndege wa Amani kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani duniani jijini Dar.

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC_1196.jpgMgeni Rasmi Mzee Mwinyi akihutubia wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa sherehe za Siku ya Kimataifa ya Amani leo asubuhi jijini Dar. Kulia ni balozi wa Rwanda nchini Ben Rugangazi na kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) Jama Gulaid.
 
Meza kuu.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC_1130.jpgBaadhi ya wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jijini wakitumbuiza kwa nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kudumisha Amani na upendo duniani.
 
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa ofisi za mabalozi waliohudhuria sherehe hizo kwenye ukumbi wa Don Bosco.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2013/09/DSC_1143.jpgBaadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.

.awaasa vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao

.ashangaa wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi za miaka 1990s

Na.Mo Blog Team

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan
Mwinyi amesema kuna baadhi ya watu katika jamii hutumia elimu, ujuzi
na maarifa yao kuangamiza, kubomoa na kudumaza Ustawi wa Jamii kwa
maslahi binafsi na si ya Umma. Mo blog inaripoti.

 

Mzee mwinyi amesema hayo wakati wa kuadhimisha siku
ya Kimataifa ya Amani Duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka
ambayo imefanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam,
amesema kuna baadhi ya watu wanatumia elimu yao vibaya kwa kupanga
kuua watu wengine kwa maslahi yao aidha ya kisiasa au ya
kiuchumi.

“Elimu kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii
husika endapo itatumika sawia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa
maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla, ila kuna baadhi ya wanajamii
kutumia ujuzi huu vibaya na kuangamiza ustawi wa jamii husika,”
amesema.

Mzee Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika
kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani duniani yenye kauli mbiu
“Education for Peace” ni lazima elimu kwa ajili ya amani iwe endelevu
hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na utengamano katika jamii na
mataifa yote duniani.

Amesema kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa
na wanasiasa kwa maslahi yao ya kisiasa na wajifunze kutatua matatizo
yao kwa njia ya amani bila ya kuwa na mihemko, jazba, misongo na
hasira ili kuendelea kudumisha amani na upendo katika nchi yetu ambayo
ni kisiwa cha amani.

“nawaasa vijana wakitanzania wa leo hata kama
mmenyimwa haki zenu ni bora kutumia njia ya kistaarabu na kutumia
elimu mnayopata mashuleni bila kusahau macho, masikio na vipawa vyenu
mlivyopewa na mwenyezi mungu katika kutafuta haki yenu kwa njia ya
amani bila misukosuko,” aliongeza.

Mzee Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi
ya watu kwa kutumia ujuzi na elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa
bila yeye kujua wametumia muktha gani kumpa jina hilo, lakini Mzee
Mwinyi alitumia jukwaa hilo pia kuwapa ruksa vijana kutumia elimu yao
kuleta hali ya amani na utulivu ndani ya nchi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja
wa Mataifa uliweka maazimio siku ya kimataifa ya amani duniani ili
watu wanaogombana na kupigana kwa shida mbalimbali kupata nafasi ya
kuweka silaha zao chini katika siku hii adhimu.

Amesema kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa
mwaka 1982 kwa mara kwanza linatambua uwepo wa watu wanaoathirika na
vita katika sehemu mbalimbali duniani na waliokwishapoteza maisha
kutokana na matatizo vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Naye Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na
vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala
la amani na utulivu linaanzia kwenye kaya hadi ngazi ya taifa kwahiyo
ni muhimu kwa jamii na vijana kuelewa amani inaanzia
nyumbani.

“jamii iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi
kubwa ya kuleta matokeo chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla
lakini jamii iliyolelewa vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu
ni zao la tunda baya,” alisema.
Mdachi alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili
ndani ya jamii ya leo swala hilo pia lilianzia kwenye kaya ya mtu
mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa ambapo leo hii taifa linashuhudia
mambo ya kifisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma kunakofanywa
na viongozi waandamizi.

Rais Kikwete akabidhi hati za utambulisho kwa maBalozi wa heshima wa Tanzania Washington DC





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa serikali yake inajitahidi katika kuboresha hali ya uzalishaji wa bidhaa nchini Tanzania, lakini bado kuna hitaji la wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania katika kuboresha huduma na bidhaa zinazopatikana nchini humo na kuziuza kama bidhaa zilizo tayari kwa matumizi badala ya bidhaa-ghafi.

Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa jumatano wiki hii wakati akiwahutubia watu waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi hati kwa mabalozi wa heshima wa Tanzania kutoka majimbo mbalimbali ya nchini Marekani, sherehe zilizofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini  Washington DC

Sikiliza ripoti hii ambayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30am). Hii ilikuwa ripoti ya Septemba 21, 2013.


Rais Kikwete awasili New York kuhudhuria Kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 22, 2013 | 8:31 PM


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Mhe. Haroun A. Suleiman.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York,
 
 Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Iadara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya JW Marriot ya Jijini New York, Marekani. Mhe. Rais Kikwete na Ujumbe wake yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinachofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) naye akiwasili katika Hoteli ya JW Marriot akiwa amefuatana na Balozi Mushy (kulia) pamoja na Msaidizi wake Bw. Togolani Mavura.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
Na Rosemary Malale, New York


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.


Kikao hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General Debate) ni “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.


Pamoja na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe. Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo:- Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.


Mingine ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.


Katika hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa Makampuni mbalimbali.


Aidha, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na Kamati ya masuala ya Sheria.


Viongozi wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman; Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).
Wengine ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger