Rais Kikwete azindua Mpango wa Kuzishirikisha Sekta mbalimbali kupambana na Malaria - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » Rais Kikwete azindua Mpango wa Kuzishirikisha Sekta mbalimbali kupambana na Malaria

Rais Kikwete azindua Mpango wa Kuzishirikisha Sekta mbalimbali kupambana na Malaria

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, September 25, 2013 | 5:49 PM



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuAV6dDhIgTw_dUxlx5JEReti4GkuiXwTyxfd0uwJI8Wry6j0wI7PSvRueZBknrXnU3d7-zWWzeaNQx2Mjki8mIFootAEJ7c5cWfoJJCqYk8xKX__X2D2gSGh9mkzGPIHFKPK4pRn5oRcs/s1600/0L7C0016.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8QYccPbq2sfrf-Qm9CddccpJ2-TDwkLsgk7mPIexpOSsP7JiI5WecF6RczULIntksLBxDImRdIrJQqsWtaUc4tzAdSnGDG8TvFqsK4bd-wHHcYrpXSn0S6L_4o50hcId38ji0gmiyFf5A/s1600/0L7C0043.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kuzindua rasmi Mpango mpya wa Kimataifa utakaohusisha Sekta mbalimbali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria duniani. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani chini ya uratibu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Taasisi ya Roll Back malaria Partbership.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Waziri wa Afya na Ustawai wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi (Mb.) (kulia) wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Guebuza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuzishirikisha Sekta mbalimbali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
   Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Guebuza wakiwa na wageni waalikwa wengine.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula akiwa na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukabiliana na malaria kwa kuzishirikisha sekta mbalimbali.

Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Milenia, Prof. Jeffrey Sachs akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWJnm9x2R7sq2rAifQwtHzpm7j0GTnWUcQHenBJxL8i35UB1DXiUmpiSWRzMOc9KJ7LQOXueglxw3Ij0vtDS0lJjm3jzM5vwC72ZMQpw42qKKNiSrEYOJRAmA8LYyIYf6vY1qdVOSwG2BT/s1600/0L7C0046.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5S4zX9-5p0AH-5Gf23p0aMBaHqHwaQ0s0ncvP51fngi0MXQt6L-MRkID2Mluf4s_E9cpwtCaTxxI0MZxgSD1wda6BqsjsL_Sp_0I2G9GbBs8edhQovuJqiNnJ-q6gfrCp8Pu2cQwSbkiF/s1600/0L7C0045.jpg
Mwakilishi wa Taasisi ya Roll Back Malaria Partnership mjini New York Bw. Herve Verhoosel akimkabidhi Mhe. Rais Kikwete mfano wa kifaa cha kufukuzia mbu  wakati wa uzinduzi wa mpango wa mapambano dhidi ya malaria.

Mhe. Mwinyi akifurahia jambo na Bi. Rebeca Grynspan kutoka UNDP pamoja na Bi. Ellen Maduhu, Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania, New York.
Picha na Rosemary Malale
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger