WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU NA MKOA WA DAR ES SALAAM - Septemba 12,2013 - Sema Naye
Headlines News :
Home » » WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU NA MKOA WA DAR ES SALAAM - Septemba 12,2013

WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU NA MKOA WA DAR ES SALAAM - Septemba 12,2013

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, September 12, 2013 | 9:45 PM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa idara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam - Septemba 12,2013.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo - Septemba 12,2013. kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao masuala mbalimbali ya utendaji kazi..
Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam - Septemba 12,2013. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu) ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).

Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger