Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi yanyakua ubingwa wa Sheni Cup Zanzibar - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi yanyakua ubingwa wa Sheni Cup Zanzibar

Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi yanyakua ubingwa wa Sheni Cup Zanzibar

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 9, 2013 | 9:40 PM


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi Kipa Bora wa mashindano ya ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi.

Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohamed Haji jezi na vifaa baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa  Dr. Sheni Cup huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Balozi Seif akimkabidhi Kikombe Kepteni ya Mabanati wa Timu ya Pete ya Tusitengane ya Nungwi Ndamu Makame Mussa baada ya kuibuka na ushindi wa Kombe la Mwanamwema Sheni dhidi ya Timu ya Pete ya Tuko Imara.

Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohamed Haji akifuahia kikombe anachokabidhiwa na mgeni rasmi balozi Seif baada ya kutawadhwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.Kati kati yao ni lezi wa Jimbo la Nungwi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa wa Idara Maalum Haji Omar Kheir

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis akipokea mchango wa shilingi Milioni 2,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia ufufuaji wa michezo ya ndani inayoonekana kufifia hapa Nchini.

Hatimae Mabingwa wa Mashindano ya Ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi na kufadhiliwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni amepatikana.

Hii ni baada ya mchezo wa Fainali ya mashindano hayo yaliyozikutanisha Timu za Soka za Kitamli ya Nungwi dhidi ya wapinzani wao Timu ya Soka ya Mwendo Mdundo ya Kidoti. 

 Pambano hilo la Fainali lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa soka wa Jimbo la Nungwi na Vitongoji vyake limeiwezesha Wenyeji wa mashindano hayo Timu ya Kitamli ya Nungwi kuibuka na ushindi kwa kuilaza Mwendo Mdundo ya Kidoti Goli 1-0. 

 Timu ya Kitamli ilijipatia goli lake la pekee na la ushindi lililofungwa na mchezaji Haji Wa Haji katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambapo mgeni rasmi katika pambano hilo la Fainali ya Dr. Sheni Cup alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mashindano hayo ya ujirani mwema yaliyoanza kutimua vumbi Tarehe 24/8/2013 yamejumuisha Timu Tisa kutoka katika vijiji tofauti vya Jimbo la Nungwi yakienda sambamba na yale ya mchezo wa Pete { Net Ball } kwa Wanawake yaliyojumuisha Timu Nne. 

 Akizungumza mara baada ya pambano hilo la Fainali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwahimiza Vijana hao kujitahidi kujifunza zaidi michezo ili wajijengee njia rahisi ya kupata ajira kupitia sekta ya michezo ambayo wakati huu imekuwa na thamani kubwa Duniani.

Balozi Seif alisema Ulimwengu hivi sasa umeshuhudia ongezeko kubwa la ajira kupitia Sekta ya michezo hasa Mchezo wa soka na Table Tennis ambayo imeonekana kutajirisha wanamichezo wengi wenye vipaji vikubwa vya michezo hiyo. 

 “ Tumeshuhudia wachezaji mbali mbali Duniani wakiwemo pia wale wanaotokea Bara letu la Afrika wakicheza mpira wa kulipwa katika timu mbali mbali za bara la Ulaya hasa ndani ya Uingereza. Huo ni Mfano halisi mmaopaswa kuutilia maanani ili na nyinyi siku moja mjikute mmetinga katika vilabu hivyo maarufu Duniani “. Alisisitiza Balozi Seif.

Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger