RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZINDUA JENGO JIPYA LA KITUO CHA JAMII NA WATOTO LA ZAPHA ZANZIBAR. - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZINDUA JENGO JIPYA LA KITUO CHA JAMII NA WATOTO LA ZAPHA ZANZIBAR.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZINDUA JENGO JIPYA LA KITUO CHA JAMII NA WATOTO LA ZAPHA ZANZIBAR.

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 22, 2013 | 8:03 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimyemw3dxjCoDxpJszXYCI4gItpTjAOQFTiCIHaNraNVnINM_kHDlo78n7-xGWGTRT8aB6_PDQi75H72UveqKSduGCnREgypjZSkl40VrD56Scbqk7nwq5LuxwM44FYa_nIivf67-ETdJV/s1600/01.JPG
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akikata utepe kuzindua Jengo jipya la kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya wazamini wa kituo hicho Bi. Hasina Hamadi. Welezo nnje kidogo ya Mji Zanzibar.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjj6MEmK2XWywZT3I21yW2cIiKaB6AHV2x8YfsMkwepZJyEzxm8eyAsRxHKUjLF54eCYbxP_iGnChyfMJDp5Unihrl-GOcI6ZAu76MvcPr3iW3Q32k8OAQPm6QFOd9VD93QfRA-5_Ksjs1B/s1600/02.JPG Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akipata maelezo kwa mshauri Nasaha wa kituo cha (ZAPHA+) Salum Ramadhan Wakili alipokuwa akiangalia baadhi ya huduma zinazo tolewa kituoni hapo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiziBdSeSJyvnhGX3gijcHty-9afYJ39ekIsaXVNOBjhA2Lc5rX1c6qJLLTDJX-j9j76ae2HYSBYe0Mbj7Ui1bNMwS7nDReKx4GcTRh-RvRqALa9lb_4T9aBtFu4SKbmezVPjQBTtQeYCX8/s1600/03.JPG Wasanii wa (ZAPHA+) wakionesha igizo jinsi ya watu wenye UKIMWI wanavyo fanyiwa unyanyapaa,huko Welezo katika uzinduzi wa Jengo la  kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) Mjini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9squStUUAKOnRbFWtBysLEHwqlk2Nu2-GfC-hfLba57x_xuBzWMs-y3QjUohDnCpzq6JbJN3OSgui_o0uHfhSdOT6y9EBnvAfEWa0z9vEh218dUZ8vX0PXVIGLm__JxWQIDdAqnQaVEQa/s1600/04.JPG Baadhi ya wageni walikwa waliofika katika  uzinduzi wa Jengo la  kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) Welezo nnje kidoga ya Mjini Zanzibar.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZIgSYvSAfub2wcPNsVAoB4LgjB00DjA5Y6z8YXw1bBbKvf2r4eWdKBFApMWApEwT6AXvPZxMFjXPaiqXm2aHqZsbG8sScKheNC7LQTrepCgQAgj7tbcu98lkC9uukT_d1vvkafdZ6pFtA/s1600/05.JPG Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akiwahutubia wananchi katika uzindizi wa Jengo la (ZAPHA+) huko Welezo nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAZD7arF6ZYdGWLa4fZM0iA9RH5iqsZE72Kx1oQlR11-vDdX3EwtcO2uSlJgfaQou75EfVgLBSZf2_oEYR08fdLVD4oJ-g_lu7QCeXFCOMciICHe6KMI8jwtJVxj3xznACa9jkei55UOQd/s1600/06.JPGRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein katika picha ya pamoja na watoto wanaopatiwa huduma na (ZAPHA+) huko kituoni kwao Welezo nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar. PICHA ZOTE NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR
Na Khadija khamis na  Riziki Salum  Maelezo Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amewapongeza viongozi wa ZAPHA + kwa jitihada zao zilizowawezesha kumiliki jengo lao endelevu la kuweza kutoa huduma bora kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Zanzibar.

Kauli hiyo alitolewa jana huko katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la ZAPHA+ Kituo cha jamii na watoto  kilichopo Welezo wilaya ya Mjini Magharibi.

Alisema kuwa hatua hiyo iliyofikia ni nzuri na ya kupongezwa kwa mafanikio hayo kwani  ni chachu ya maendeleo kwa wanaoishi na maambukizo ya virusi  vya UKIMWI  katika  kujiona wanajamii kuwa na chuo chao cha kupata elimu  na ushauri nasaha  pia ni chimbuko la matumaini kwa watoto wanaoishi na  maambukizi ya UKIMWI.

“Serikali inathamini juhudi zenu za jumuiya kwani inatoa mashirikiano ya pamoja kwa kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ukimwi,” alisema Dkt Shein.

Aidha alisema kuwa zaidi ya watoto 547 tayari waneripotiwa wanaishi na virusi vya ukimwi  sawa na asilimia 68 % wakiwa wanaume 194 na wanawake 180 ambao tayari  wanatumia dawa za ARV Zanzibar.

Alisisitiza kuwa iko haja ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushirikiana katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, mayatima  na wanaoishi na virusi .

Alisema kuwa iko haja kwa wananchi kukubali kubadili  tabia zao na kurudi katika tamaduni zao za mila silka na itikadi  za kizanzibari kuweza kupendana  kushirikiana  na kusaidiana kwa hali na mali .

Aliengezea kuwa wananchi katika kushikamana tupige vita juu ya utumiaji madawa ya kulevya kwani tathmini inaonyesha kuwa  asilimia kubwa ya walioathirika ni vijana ambao wamejihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya .

Nae  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo  Consolata  John alisema kuwa amemshukuru Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein kwa kuweza kukubali mwaliko wao kwani ni ishara tosha ya kuwajali na kuwathamini sana mchango wao katika maendeleo ya jamii ya Zanzibar.

Aidha alisema kuwa juhudi kubwa zinachukuliwa katika kuendeleza jumuiya hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimabli ya kimaendeleo ikiwemo kilimo cha mboga mboga , utengenezaji wa sabuni na mafunzo ya mapishi kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi.

Jumuiya ya ZAPHA + Zanzibar imeanzishwa mwaka 1994 na kusajiliwa rasmi kama asasi ya kiraiya mwaka 1996 ikiwa na wanachama waanzilishi 26 hadi sasa ina wanachama 2022.

Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger