Home »
Label 5
» MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA
MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA
Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 23, 2013 | 1:34 PM
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo kufyatua matofali na vijana wa CCM walioweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Mji mdogo wa laela tarehe 22 Septemba 2013. Lengo kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera za Chama cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa ujumla. Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma akiwahamsisha vijana hao kukipenda chama chao kwa kuweka uzalendo mbele katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Chama hicho katika mji mdogo wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka kushoto ni Matin Matete Mjumbe wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa, Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Persin Kalikule Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.
Sehemu ya vijana hao waliotoka katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakionekana kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo iliyopo katika mji mdgo wa Laela.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao akielezea mipango mbalimbali ya umoja huo ikiwemo uhamasishaji na upandaji miti ya mbao kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi Mkoani Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na viriba vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM Mkoa wa Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la upandaji miti wa kibiashara.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.)
Labels:
Label 5
0 comments:
Post a Comment