Mh. Wasira azungumza na watumishi Mkoani Lindi - Sema Naye
Headlines News :
Home » » Mh. Wasira azungumza na watumishi Mkoani Lindi

Mh. Wasira azungumza na watumishi Mkoani Lindi

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, September 20, 2013 | 9:27 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaphmLxHbjOZNLlnO6jHy1d2eB5jHdg9Gg6xDS63O105rpf_eJXW1I8wM1YUsS0O7pI4ZMMCChJp8JfQLmzVMOE07Eq_XlaVJBuPdewQut5_gIIuilcCI7a8AXzYAiNs_pvoumvKr9CoD7/s1600/IMG_3937.JPG
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen Wasira (aliesimama) akizungumza na watumishi mkoani Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi. Na Abdulaziz Video,Lindi
 

WATUMISHI wa Serikali wakiwemo wataalamu mbalimbali,wametakiwa kuwatumikia wananchi,wakiwemo wakulima wa zao la korosho kwa kuwawekea Mfumo ambao utawapa Haki itokanayo na jasho lao.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen Wasira,ametoa kauli hiyo,alipokuwa akizungumza na watumishi mkoani Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi.

Akizungumza na watumishi hao,Wasira amesema Serikali inajipanga kufanya marekebisho ya ununuzi wa zao la korosho kwa kutumia Mfumo wa Stakabadhi mazao Ghalani,ili kumuwezesha mkulima kulipwa fedha kwa lengo la kunufaika na Jasho lake.

Wasira amesema iwapo hakutakuwa na mfumo mzuri wa kuwatendea Haki wakulima hao,ikiwemo kuwasimamia vizuri na kuwalipa fedha zao, itakuwa ni vigumu kwao kuondokana na hali ya umasikini unaowakabiri hivi sasa ndani ya Taifa lao.

Amesema iwapo watumishi ambao watashindwa kuwajibika ipasavyo kwenye maeneo yao ya kazi,hakuna sababu ya kuwapandisha vyeo au kuendelea kuwepo kazini.

“Hivi mtumishi mfano Afisa Kilimo ameshindwa kumbadilisha mkulima kutoka kilimo cha kizamani na kwenda cha kisasa,kuna muhimu gani wa kumpandisha cheo,,,,,,,,hapo asilalame kwa nini hajapandishwa Cheo licha ya kuwepo kazini kwa muda mrefu,hapo anatakiwa aseme kwa nini anaendelea kuwepo kazini bila ya kufukuzwa”Alisema Wasira.

Waziri huyo wan chi Ofisi ya Rais,Mahusiano na uratibu,amesema kamwe umasikini wa wananchi wakiwemo na wakulima hautaweza kuondolewa kwa utaraibu wa kuwaibia mazao yao,kwani kwa kufanya hivyo bado wataendelea kujengewa mazingira magumu ya maisha yao

Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger