Mh. Lowassa awataka waimbaji wa nyimbo za Injini kuhubiri zaidi Amani ya Tanzania - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » Mh. Lowassa awataka waimbaji wa nyimbo za Injini kuhubiri zaidi Amani ya Tanzania

Mh. Lowassa awataka waimbaji wa nyimbo za Injini kuhubiri zaidi Amani ya Tanzania

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, September 9, 2013 | 9:38 PM


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa ameketi kusikiliza lisala ya hafla hiyo iliyokuwa ikisomwa na Bahati Bukuku (hayupo pichani) huku umati wa waumini wakifatilia kwa umakini.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiombewa na mchungaji Katunzi wa EAGT pamoja na waumini wengine,wakati wa hafla ya uzinduzi wa albamu ya Nyimbo ya Injili iitwa Dunia,iliyoimwa na Mwanamama Bahati Bukuku.

Muchungaji wa kanisa la EAGT City Center,Florian Katunzi (mwenye kipaza sauti) akiombea baadhi ya cd za album ya Bahati Bukuku iitwayo dunia,Kabla ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa (katikati).Watatu kulia ni mwimbaji huyo Bahati Bukuku.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha Harambee hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya watu wakati alipokuwa akiondoka ukumbini hapo.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa amewataka waimbaji wa nyimbo za injili nchini, kuhubiri zaidi amani ya Tanzania katika tungo zao.

Lowassa aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa album ya mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili hapa nchini,Bahati Bukuku iitwayo dunia,wakati wa Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba waimbaji wa injili, kuhubiri zaidi amani ya nchi yetu,amani ni muhimu sana jamani,mkitumia kipaji chenu hiki kuhubiri amani, taifa letu litaendelea kuwa na Umoja,upendo na mshikamano" alisema Lowassa huku akishangiliwa na maelfu ya waumini wa kanisa la EAGT city center pamoja na wananchi wengine.

Awali katika risala yake, Bahati Bukuku alisema ameanzisha kampuni ya kurekodi na kusambaza Kazi za waimbaji wa nyimbo za injili, hivyo anahitaji msaada kufanisha lengo lake hilo.

Moja wapo ya hatua za kufanikisha lengo lake hilo, ni kufanyika kwa Harambee sambamba na uzinduzi huo, ambapo Mh Lowassa na mkewe walichangia shilingi milioni kumi, marafiki zake watatu, akiwemo Philemon Mollel, Anoj Shaha ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda Cha A to Z waliyotoa milioni tano kila mmoja.
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger