Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina pamoja na wazazi wa mbunge huyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka
mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini
kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza
kero za wananchi mitaji na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia
wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la
moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya
Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa kupita
kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa
na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.
0 comments:
Post a Comment