JK AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MWANZA NA KUHUTUBIA WANANCHI WA MAGU - Sema Naye
Headlines News :
Home » , » JK AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MWANZA NA KUHUTUBIA WANANCHI WA MAGU

JK AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI MWANZA NA KUHUTUBIA WANANCHI WA MAGU

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 8, 2013 | 5:04 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMntCbsC7k1EAa5eOxaAoLt5FknRBABXAteFzTDs4f68tnUFheh4rCNluzlh2BsKHZKTDx1glQN3FjfAchSUPA7nAqZK_LvcBi5lABIpXHSAwOQPb15sZX95bRsExFbcEQcUeQAcjkEXHp/s1600/0L7C0085.jpg
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafurahia wasanii chipukizi Gosbert Bwere(4) anayepiga ngoma na mwenzake Nyambari Mganga(5) walipokuwa wanamtumbuiza muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nansio,Ukerewe, kwa ziara ya kikazi.
----------------------------------------

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jaqueline Liana, (kushoto,) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (katikati) mara baada ya kuwasiri katika makao makuu ya kata ya Lugeye ambako kulitolewa taarifa ya wilaya ya Magu
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma ya wananchi wa kabila la Wasukuma wanayocheza na nyoka aina ya chatu wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye iliyopo wilayani Magu. Zahanati hiyo imegharimu kiasi cha  milioni 170.
 
Wananchi wakishuhudia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Shadrack Faustino Mbilizi aliyehudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye huko Magu na pia alipokea kupokea kadi yake ya kitambulisho cha matibabu kwa wazee .
Rais Jakaya Kikwete akipokea kitambulisho cha matibabu kwa wazee kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jaqueline Liana kwa ajili ya kupewa Kanali Mstaafu Shadrack Mbilizi na mkewe Mariam Said wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye

 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kata ya Lugeye wakati wa sherehe za kufungua jengo la zahanati ya kata hiyo.
 
Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la  Ilungu karibu na mji wa Magu.  Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika.
 
Rais  Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu.
 
Rais  Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Picha zote na John Lukuwi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siyo kazi ya Serikali kuviokoa

vyama vya ushirika kutoka kwenye madeni kwa sababu shughuli za ushirika ni za

sekta binafsi na mali ya wanachama wenyewe.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa makosa ya ushirika na wezi wa baadhi
ya viongozi wa vyama vya ushirika hatimaye yanabebeshwa vyama vya siasa.
Kama namna ya kuwasaidia wananchi, Rais Kikwete amewataka viongozi mbali mbali wa mikoa
kuwasaidia wananchi ili kupata viongozi waadilifu na waaminifu na wala siyo
wezi kama ilivyo sasa kwa vyama vingi vya ushirika.
Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 7, 2013, wakati
alipopokea Ripoti ya Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwenye Ikulu Ndogo mjini
Mwanza kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.
Rais Kikwete aliwaambia viongozi hao wa Mkoa wa Mwanza: “Tumewahi huko nyuma kulipa madeni
yote ya vyama vya ushirika. Nia ilikuwa kuvisaidia vyama hivyo na wanachama
wake kujipanga upya na kupata uhalali wa kuweza kukopa fedha za kjuendesha
shughuli zao. Lakini sasa, vyama hivyo, vimerudi kule kule kwenye madeni.”
Alitoa mfano wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani kama moja
ya vyama vya ushirika ambavyo madeni yake yalilipwa na Serikali lakini sasa
kina deni kubwa zaidi kuliko hata lile lililolipwa na Serikali.
“Wale watu wa Pwani walikwenda kukopa na benki moja ikakubali kuwapa fedha. Wameshindwa
kulipa na ule ushirika nadhani utakufa. Njia bora kwa vyama vya namna hiyo ni
kuviachia vife tu kwa sababu havina faida yoyote kwa mkulima.”
Aliongeza:
“Vyama vya ushirika siyo mali ya Serikali. 
Ni mali ya wanaushirika na hivyo ushirika ni sekta binafsi. Lakini hakuna shaka kuwa
baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanatesa wananchi. 
Wanakopa fedha kwenye mabenki lakini wanashindwa kuzirudisha fedha hizo na hilo 
linapotokea Serikali inalaumiwa kwa hali hiyo.”
Rais alikuwa anatoa maelekezo yake baada ya kuambiwa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza cha
Mkoa wa Mwanza kilikuwa kinakamilisha mpango wa kukopa kiasi cha sh bilioni
saba kutoka Benki ya Raslimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununulia pamba.
Lakini aliwaambia viongozi hao: “Uamuzi wa kukopa ama kutokukopa ni wa kwenu. 
Nyanza ni mali yenu, wezi waliopata kukibebesha madeni chama hicho mliwachagua nyie wenyewe.
Fedha ni zenu lakini hatimaye athari za makosa yenu yanaiathiri Serikali na
hata vyama vya siasa.”
“Kuna wakati viongozi wa Chama cha Nyanza walipata kuuza godown ya thamani y ash milioni 600
kwa sh milioni 50 tu. Hawa ni wezi wa mchana wanaoiba kweupe. Wanaiba lakini
wanataka Serikali iwasaidie. Kwa nini? Nadhani kazi yetu kama
viongozi ni kuwasaidia wananchi kupata viongozi adilifu na aminifu siyo wezi,”
alisema Mheshimiwa Rais Kikwete na kuongeza:
“Tatizo ni kwamba
hata sisi viongozi tunakataa kuwashughulikia wezi kwa sababu hawa ni watu
maarufu na wakati mwingine baadhi ya viongozi wanakula nao na jambo hilo limekuwa tatizo kubwa sana. 

Tunavifikisha vyama vya ushirika mahali
ambako sina uhakika kama bado ni mali ya wakulima. Wakulima
wanakutana na ushirika wakati wa kuchagua viongozi tu na baada ya hapo wakulima
hawaonekani tena.”
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger