January Makamba azindua tume ya tehama leo Jijiini Dar. - Sema Naye
Headlines News :
Home » » January Makamba azindua tume ya tehama leo Jijiini Dar.

January Makamba azindua tume ya tehama leo Jijiini Dar.

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, September 12, 2013 | 9:49 PM


Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (wa pili toka kushoto mstari wa mbele), wa kwanza wake toka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Bi. Clarence Ichwekelezwa na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu. 

Mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe.January Makamba akitoa salamu zake kwa wadau mbalimbali (hawako pichani) waliohudhuria mkutano kabla ya kutoa hotuba yake wakati alipokuwa  akizindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo.  



Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Mkutano wa wadau  juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA wakifauatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi . Mkutano huo umefanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. 

Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba akijibu maswali mbalimbali toka kwa waaandishi wa habari mara alipomaliza kuzindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam.
.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.


======= =====  ======

UZINDUZI WA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA TUME YA TEHAMA.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

12/09/2013.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba amezindua rasmi mkutano wa Washikadua juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA leo jijini Dar es Salaam.¨




Mhe. Makamba amesema kuwa TEHAMA kitakuwa chombo kikubwa ambacho kitashirikisha wadau wengi hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanasonga mbele na inatoa fursa mbalimbali zenye kuweza kutatua changamoto za kimaisha kwa watanzania.




Mhe. Makamba aliongeza kuwa TEHAMA ndiyo inaleta mabadiliko na kuleta maendeleo makubwa hivyo amesisitiza juu matumizi ya TEHAMA katika ofisi za serikali na sekta binafsi. Aidha, amewashauri wadau wote kuangalia wenzetu nchi zilizoendelea jinsi wafanyavyo ili kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yanasonga mbele. “Kama Taifa hakuna sehemu ambapo tunakutana kutafakari juu hali ilivyo katika matumizi ya TEHAMA hapa nchini”. Alisema Mhe. Makamba.




Kwa upande mwingine Mhe. Makamba alisisitiza juu ya wanataaluma wa TEHAMA wawe wanajulikana na amesema kuwa katika uundaji wa Tume hiyo ni vema wataalamu na ufanisi wa kazi zao ujulikane ili kuepukana na kuwa na wataalamu ambao ni Makanjanja. “Hapa nchini Tanzania hatuna uhakika wa wahitimu katika mambo ya TEHAMA hivyo kuna uwepo wa vyuo na tasisi ndogondogo nyingi zilizosambaa ambazo zinajikita kutoa taaluma hiyo, katika masuala ya TEHAMA ni lazima wataalamu wajulikane na kusajiliwa kama ilivyo katika bodi nyingine za serikali hapa nchini”. Alisema Naibu Waziri.




Aidha, Mhe. Makamba alimalizia kwa kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayofanya kwa upande wa TEHAMA kwani mpaka hivi sasa nchi imefikia mahali pazuri katika mambo ya mawasiliano pia ameshauri juu ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uundaji wa tume ya TEHAMA. 
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger