TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LATUMBUIZA WAKAZI WA MTWARA
Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, August 31, 2013 | 10:49 PM
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Baba Levo akiwaimbisha wakazi wa Mtwara wimbo wake uitwao Polisi,usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Ni shangwe za kutosha usiku huu ndani uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Msanii aliyeibuka kwa kasi hivi sasa katika muziki wa Bongofleva,aitwaye Snura akionesha staili ya Kuvurugwa jukwaani usiku huu.
Baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Mtwara na vitongozji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona usiku huu.
Anaitwa Dj Mully B akionesha umahiri wake wa kukamua mangoma mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 usiku huu.
Mashabiki wa tamasha la burudani la Serengeti Fiesta 2013 wakifuatilia kwa makini yanayojiri kwenye tamasha hilo usiku huu ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara,ambapo wakazi wa mkoa huu kwa mara ya kwanza walishuhudia live tamasha hili ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Wakishangweka safi kabisa usiku huu.
Ni burudani ya kutosha kabisa usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta ambapo maelfu ya watu wamejitokeza kuburudika ndani ya uwanaj wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Anaitwa Linah kutoka nyumba ya vipaji ya THT,akiimba jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Mtwara waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Kijana mdomo,lakini anaonekana kuja kwa kasi kabisa katika anga ya muziki wa kizazi kipya,hasa hip hop,aitwa kwa jina la kisanii Young Killer kutoka jijini Mwanza,akitumbuiza usiku huu mkoani Mtwara kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
PICHA NA MICHUZIJR.BLOGSPOT
0 comments:
Post a Comment