Picha za Swala ya Iddi Unguja leo - Sema Naye
Headlines News :
Home » » Picha za Swala ya Iddi Unguja leo

Picha za Swala ya Iddi Unguja leo

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, August 9, 2013 | 12:26 PM




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid karume kabla ya kuanza kwa Swala ya Idd el Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman,Mjini Unguja. Kati yao ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
 
 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ,akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kitaifa iliwaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja leo katika kufuatia kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 
 Sehemu ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala ya Idd el Fitri,iliyoswaliwaa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan
 
 Akina mama waumini wa Dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idd el Fitri katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan
 
  Imamu Mkuu wa Msikiti Masjid  Mushawal Mwembeshauri Sheikh Mziwanda Ng'wali Ahmed,akitoa hutuba ya swala ya Idd el Fitri,katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Ungujaleo katika kusherehekea sikukuu hiyo kwa wailamu wote Duniani
 
 Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi el fitril.
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger