PICHA; YALIYOJIRI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA...!! - Sema Naye
Headlines News :
Home » » PICHA; YALIYOJIRI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA...!!

PICHA; YALIYOJIRI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA...!!

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, September 1, 2013 | 11:53 PM



Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika kumuanga SHUJAA WA INJILI Dr Moses Kulola aliyefariki 29 Agosti saa 5.30 hapa jiji Dar.


Kati ya watu ambao wamekuwepo katika ibada hii ya kuuaga mwili wa Dr Askofu Moses Kulola, wamehuduria watumishi wa Mungu mbalimbali ikiwa ni pamoja na 

Maaskofu, Wainjilisti Mitume na Manabii.

Askofu kulola alizaliwa mkoani Mwanza, mwaka 1930 na kufariki 29 agost 2013.

Baadhi ya watumishi
Katika uhai wake mzee Kulola alifanya kazi ya Injili hadi kifo kinamchukuwa, ila kati ya kazi aliyoifanya ni pamoja na kutembea kwa mguu kutoka Mza hadi Mtwara. Lakini pia safari nyingi alizozifanya zilikuwa katika mazingira magumu. Amehubiri injili ndani na nje ya nchi.
Mama Kulola (Mjane

Mtoto wa Mzee Kulola Willy, akilia kwa uchungu

 Askofu Silvester Gamanywa akimpa pole mama Kulola

Watumishi wa Mungu mbalimbali wakisubiria mwili wa Dr Moses Kulola

Msafara wa mwili wa marehemu Dr Mose Kulola ukiwasili katika viwanja vya Temeke


Waimbaji mbalimbali walikuwepo 
 Baadhi ya ndugu kutoka Mza 
Mchungaji Lwakatale akiandika kwenye kitabu cha waombolezaji
Watumishi wengi walifika kwa ajili ya kuuaga mwilia wa aliyekuwa shujaa wa Injili Tz Dr Moses Kulola
Mchungaji  Getrude Lwakatare wa Mikocheni Asb. of God
Mchungaji Antony Lusekelo
Askofu Silvester Gamanywa
Watumishi wengi mbalimbali waliopata nafasi ya kuelezea jinsi walivyomfahamu Dr Kulola, walisifu jinsi alivyokuwa akipiga injili isyokuwa na ubaguzi wala upendeleo.
Miongoni mwa watu waliofika na kueleza jinsi  walivyomfahamu Mzee Kulola  ni Makamu Mwenyekiti Bara wa CCM Mzee Philip Mangula, ambaye amekuwa msaada mkubwa katika maisha yake ya kazi.
Na hata akampa mtoto wake jina la Mzee kulola ( Moses)
Lakini pia kwa niaba ya jeshi la polisi, Adivela Senso ameeleza jinsi Mzee Kulola alivyoweza kulisaidia jeshi la Polisi pindi yanapotokea matukio ya ki ualifu, na mzee alienda sehemu zenye shida na kufanya mikutano ya injili.
Anthony Joseph mtangazaji wa WAPO Radio akitoa heshima zake za mwisho, nyuma ni Obedy Kikao mtangazaji wa Upendo FM radio
Ilikuwa ni siku ya Watumishi wa Mungu kukutana pamoja
Viongozi wa chama na selikari nao pia walikuja kuaga shujaa wa Imani

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Adivera Senzo aliliwakirisha jeshi hilo katika 
msiba huu mkubwa
Makamu wa Rais Gharib Bilali akiwasiri katika kanisa la EAGT tayari kwa ajili ya kuja
 kutoa heshima za mwisho.
Share this article :

0 comments:

 
Support : 255-272-545-994 | Jasper A.K. | Mas Template
Copyright © 2011. Sema Naye - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger